Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dk Mwinyi, vigogo Real Madrid wajadili kuinua vipaji Zanzibar

Muktasari:

  • Dk Mwinyi aliyasema hayo jana Oktoba 13, 2026, jijiji Madrid nchini Hispania, katika hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo, inayolenga kuanzisha programu maalumu za mafunzo ya soka kwa vijana Zanzibar.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, anaamini soka la Zanzibar na Tanzania litapiga hatua kubwa kupitia ushirikiano baina ya miamba ya soka duniani, Real Madrid na taasisi ya Unicorn Zanzibar Sports Limited ya Zanzibar.


Dk Mwinyi aliyasema hayo jana Oktoba 13, 2026, jijiji Madrid nchini Hispania, katika hafla ya utiaji saini wa hati ya makubaliano baina ya taasisi hizo, inayolenga kuanzisha programu maalumu za mafunzo ya soka kwa vijana Zanzibar.


Rais Mwinyi, alisisitiza kuwa kipaji pekee hakitoshi kumfikisha kijana kwenye mafanikio bila mwalimu bora, nidhamu, elimu,miundombinu na mfumo unaotambua na kuendeleza uwezo wake.

"Serikali imeendeleza zaidi ya viwanja 30 vya mpira wa miguu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, na hatua inayofuata ni kuunganisha uwekezaji wa maarifa, mbinu za ufundishaji na uzoefu wa kimataifa ili kuwasaidia vijana kufikia uwezo wao,"alisema


Ameeleza, kuwa dhamira ya Serikali ni kuhakikisha vijana wanapata mazingira yanayowawezesha kukuza vipaji na kutimiza ndoto zao.


Aidha, alisema mafanikio ya programu hizo hayatapimwa kwa idadi ya vijana watakaokuwa wachezaji wa kulipwa pekee, bali kwa mchango wake katika kuwajengea nidhamu, kujiamini, kuheshimu wengine na kuwa na dhamira ya kutimiza malengo yao.