Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha ataja kinachoitesa JKT Tanzania, Polisi Tanzania

JKT Pict

Muktasari:

  • JKT Tanzania imecheza mechi nne za Ligi Kuu Bara msimu huu, ikianza na sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya TRA United. 

MWANZO usiokuwa mzuri wa kikosi cha JKT Tanzania kwenye Ligi Kuu Bara msimu huu, umemfanya kocha mkuu wa kikosi hicho, Ahmad Ally kutaja mambo yaliyowapunguzia kasi, huku akisisitiza kwamba ugumu wa ratiba unaendelea kuwatesa.

JKT Tanzania imecheza mechi nne za Ligi Kuu Bara msimu huu, ikianza na sare ya bao 1-1 nyumbani dhidi ya TRA United. Baada ya hapo, ikapoteza mechi mbili mfululizo ugenini dhidi ya Polisi Tanzania (2-0) na Yanga (4-0), iliporudi nyumbani, ikashinda 2-1 dhidi ya Namungo, hivyo kukusanya pointi nne katika mechi nne.

Kocha Ally amesema, kuna utofauti mkubwa kati ya msimu huu na uliopita na kinachowafelisha kwa sasa kiko nje ya uwezo wao ndio maana wanaendelea kupambana.

JK 01

“Unajua msimu uliopita kulikuwa na utofauti mkubwa kuanzia kwenye maandalizi mpaka ratiba za mechi kwa upande weti ukilinganisha na ilivyo sasa hivi, ndio maana tumeanza kwa ugumu kidogo.”

Amesema kuwa, jambo la kwanza linalowakwamisha ni ugumu wa ratiba, akieleza kwamba timu inasafiri umbali mrefu bila mapumziko.

JK 02

“Tunasafiri umbali mrefu na ratiba inakimbia ndani ya saa 72 mnatakiwa mcheze mechi nyingine na mnategemea kusafiri kwa basi, safari zingine zinachukua hadi saa 24 njiani. “Wachezaji wanafika wamechoka na wanaingia kwenye mechi nyingine halafu mbaya zaidi wapinzani wetu muda mwingine hawakua na ratiba ya kutoka, hivyo unawakuta wana nguvu sana,” amesema.

Ameongeza kuwa, JKT Tanzania haikupata muda wa kutosha kujipanga vyema kwenye kipindi cha maandalizi ndio maana wachezaji wengi wanaonekana kama hawako fiti.

JK 03

“Unajua tumepata muda mdogo sana wa maandalizi kuliko msimu uliopita ndio maana wachezaji wanaonekana kama hawako sawa kimwili, hizo zote ni sababu ambazo ziko nje ya uwezo wetu lakini tunajitahidi kujiweka sawa.”