Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kocha aibuka na mawili Coastal Union

COASTAL Pict

Muktasari:

  • Coastal Union ilikuwa na moto msimu uliopita ikimaliza ya nane kwa pointi 36 na kifika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (CRDB) kabla ya kutupwa nje na Simba kwa kipigo cha mabao 4-0.

KOCHA Mkuu wa Coastal Union, Fikiri Elias amesema wakati akiendelea kusuka na kuipa makali timu hiyo, anahitaji kufuta rekodi ya kuruhusu bao kila mechi pamoja na kutengeneza nafasi na kuzitumia.

Coastal Union ilikuwa na moto msimu uliopita ikimaliza ya nane kwa pointi 36 na kifika nusu fainali ya Kombe la Shirikisho (CRDB) kabla ya kutupwa nje na Simba kwa kipigo cha mabao 4-0.

Kwa sasa ‘Wagosi’ hao wamecheza mechi 11 na kuvuna pointi 14 na kuwa nafasi ya 11 na Novemba 21 watakuwa uwanjani kuwakabili Pamba Jiji,  CCM Kirumba jijini Mwanza.

PAMB 01

Akizungumza na Mwanaspoti kocha huyo amesema kwa sasa anakomalia mambo mawili akianza na kufuta tatizo la kuruhusu idadi kubwa ya mabao pamoja na kutengeneza nafasi na kuzitumia ili kujiweka pazuri.

Amesema idadi ya mabao 15 waliyoruhusu si nzuri sana na anahitaji kuanzia mchezo dhidi ya Pamba Jiji aone wakifunga bila kuguswa wavu wao, akitamba inawezekana kutokana na maandalizi waliyonayo.

PAMB 02

“Tunaendelea na mazoezi tukifahamu ugumu wa mechi inayofuata, siangalii tu kasi ya ufungaji mabao kusuasua bali natazama pia kutoruhusu mabao, kwa mechi kadhaa tumefungwa mno.”