Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KMKM yapoteza mechi ya kwanza

PEMBA. MABAO mawili yaliyofungwa kila moja katika kipindi yameizamisha KMKM kwa mara ya kwanza katika Ligi Kuu ya Zanzibar (ZPL) baada ya jana kuonyolewa na Mafunzo kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.
Licha ya kipigo hicho cha kwanza kwa watetezi hao wa ZPL, KMKM bado imesalia kileleni mwa msimamo wa ligi hiyo yenye timu 16 ikiwa na pointi 36, tatu zaidi na ilizonazo Mafunzo na JKU zinazofuata nyuma yao.
Mafunzo iliyomaliza mchezo huo ikiwa pungufu baada ya mchezaji wake mmoja kupewa kadi nyekundu, iliandika bao la kwanza dakika ya ya 29 kupitia Rashid Abdallah.
Bao hilo lilidumu hadi mapumziko licha ya KMKM kucharuka kutaka kulisawazisha na kipindi cha pili kilipoanza, Mafunzo waliotumia mfumo wa 3-5-2 iliwakimbiza wapinzani wao waliokuwa wakitumia mgumo wa 4-3-3.
Juhudi zao zilizaa matunda katika dakika ya 79 baada ya Rashid Is'haq kufunga bao la pili lililonyong'onyesha juhudi za Mabahari wa KMKM, ambao walikuwa hawajaonja kipigo katika mechi zao 16 za awali, ikishinda 10 na kutoka sare 6.
Katika pambano jingine la mapema uwanjani hapo lililopigwa Uwanja wa Amaan mjini Unguja, Zimamoto iliwazima Wakombozi wa Ng'ambo, Taifa Jang'ombe kwa mabao 2-0.
Mabao hayo yaliwekwa kimiani na Haruna Jabir dakika ya 27 na Ali Kulwa 'Makelele' dakika ya 88.
Ligi hiyo inatarajiwa kuendelea tena leo kwa mchezo mmoja tu, wakati Machomane itakapokuwa wenyeji dhidi ya KVZ kwenye Uwanja wa Gombani, kisiwani Pemba.