Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Simba Queens ajipa kazi ya kufanya

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Tangu ajiunge na timu hiyo msimu uliopita amekuwa kiungo muhimu akiisaidia Simba kubeba mataji mawili, moja la ligi na lingine la Ngao ya Jamii.

KIUNGO wa Simba Queens, Fasila Adhiambo amesema ana kazi ya kufanya msimu huu ili kuboresha kiwango chake na mwanzo wake katika mashindano ya Ngao ya Jamii haukuwa mzuri kama alivyotarajia.

Adhiambo amesema kila msimu anapoanza huwa anajiwekea malengo binafsi ya kuimarisha kiwango chake, lakini safari hii anapaswa kuongeza juhudi ili kuhakikisha anarejea kwenye ubora anaoutaka.

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo huyo amesema bado hajaanza vizuri kwenye mashindano hayo, lakini anaamini ana nafasi ya kurekebisha na kuonyesha uwezo wake Ligi Kuu ya Wanawake itakapoanza.

“Sijaanza vizuri. Huwa najiwekea malengo kila msimu unapoanza, kwenye mashindano ya Ngao ya Jamii sijaanza vizuri, lakini bado nina nafasi ya kurekebisha kwenye ligi,” amesema Adhiambo.

“Mashabiki wa hapa wamekuwa wakituunga mkono sana kuanzia tunapofanya vizuri na hata kwenye wakati mgumu kwahiyo wanatupa hamasa sana na naamini tutafanya tena vizuri msimu huu.”

Kiungo huyo ambaye huu ni msimu wake wa pili kuitumikia Simba Queens akitokea Ulinzi Starlets ya nchini kwao.

Tangu ajiunge na timu hiyo msimu uliopita amekuwa kiungo muhimu akiisaidia Simba kubeba mataji mawili, moja la ligi na lingine la Ngao ya Jamii.

Kabla ya kuitumikia Simba akiwa kwenye Ligi Kuu Kenya, kiungo huyo alifunga mabao saba na kutoa asisti 17.