Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Simba awataja Chama, Libasse

KIBAILA (1)

Muktasari:

  • Mbali na Chama, kijana huyo aliyezaliwa Januari 7, 2008, aliwataja pia Libasse Gueye na Anicet Oura ambao wamekuwa na kiwango bora msimu huu Simba na wamemsaidia kwa kiasi kikubwa hadi kuonyesha kiwango cha juu alipokuwa na Ngorongoro Heroes.

KIUNGO wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, Bashiri Kibaila amesema anajifunza vitu vingi kutoka kwa kiungo wa Simba, Clatous Chama kutokana na ubora na uzoefu alionao kwenye soka la Tanzania.

Akizungumza na Mwanaspoti Kibaila ambaye yupo katika kikosi cha wakubwa cha Simba, alibainisha kila dakika anayopata nafasi ya kucheza huwa anapewa sapoti kubwa na kuelekezwa mambo mbalimbali na mwamba huyo kutoka Zambia.

Mbali na Chama, kijana huyo aliyezaliwa Januari 7, 2008, aliwataja pia Libasse Gueye na Anicet Oura ambao wamekuwa na kiwango bora msimu huu Simba na wamemsaidia kwa kiasi kikubwa hadi kuonyesha kiwango cha juu alipokuwa na Ngorongoro Heroes.

KIBA 01

"Kila dakika ninayopata kucheza au kuwa nao uwanjani, Chama amekuwa ananipa sapoti na kunielekeza vitu vingi vya kiufundi. Ni fursa kubwa kwangu kujifunza kutoka kwake kwa sababu ana uzoefu na historia kubwa," amesema Kibaila na kuongeza.

"Pia kiwango bora cha Gueye na Oura msimu huu kimenisaidia sana kuongeza kujiamini na matunda yake yameonekana hata nilipokuwa na timu ya taifa ya vijana wapo wengi kwa karibu wachezaji wote wamekuwa na msaada mkubwa kwangu."

KIBA 02

Kibaila alikuwa mmoja wa wachezaji wenye mchango mkubwa akiisaidia Ngorongoro Heroes kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika za Vijana (AFCON U-20) mwakani nchini Ghana.

Katika mechi hizo za kufuzu, mchezaji huyo alifunga mabao mawili na kutoa pasi mbili za mabao, mchango uliowavusha vijana hao kuelekea Ghana.