Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Simba ataja ubora wake, ahadi yake kwa Kagere

KIUNGO Pict

Muktasari:

  • Mnunka ambaye ni mmoja wa wachezaji muhimu kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba, alifunga bao la kwanza na kusaidia timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kubeba taji hilo linalotetewa na JKT Queens.

KIUNGO mshambuliaji wa Simba Queens, Aisha Mnunka ameanza kampeni ya mashindano ya Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) vizuri baada ya kufunga bao katika ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Top Girls ya Burundi katika kundi C, kwenye Uwanja wa Kigali Pele, Rwanda, huku akifichua ahadi aliyompa straika wa zamani wa Simba, Meddie Kagere.

Mnunka ambaye ni mmoja wa wachezaji muhimu kwenye safu ya ushambuliaji ya Simba, alifunga bao la kwanza na kusaidia timu hiyo kujiweka katika nafasi nzuri ya kubeba taji hilo linalotetewa na JKT Queens.

Hata hivyo, baada ya kufunga bao hilo, Mnunka hakushangilia kwa staili aliyokuwa ameahidi kufanya. Awali alikuwa amemwambia Kagere akifunga bao angeiga staili yake kwa kuziba jicho moja, lakini baada ya kupata bao hilo alisahau kutekeleza ahadi hiyo.

Badala yake, Mnunka alichukua jezi ya mchezaji mwenzake, Elizabeth Wambui na kuiinua wakati wa kushangilia bao hilo. Wambui alipata jeraha la goti akiwa Kenya wakati Simba ilipokuwa ikiendelea na maandalizi ya mashindano ya CECAFA ya kuwania kufuzu Ligi ya Mabingwa Afrika.

Akizungumza baada ya mechi hiyo, Mnunka amesema ahadi hiyo aliitoa kwa Kagere siku moja kabla ya mechi, lakini furaha ya kufunga ilimfanya asahau kutekeleza staili hiyo, huku akisisitiza alichofanya kwa Wambui kilikuwa ni sehemu ya kumuunga mkono mpambanaji huyo .

“Jana wakati Kagere amekuja akaniambia kesho tunafanyaje, nikamwambia nitafunga goli na nitashangilia kama wewe, lakini nikasahau. Nisamehe bure, lakini nilishangilia nikishika jezi ya Wambui kwa sababu ni mpambanaji mwenzetu na nilimuahidi tutapambana kwa ajili ya timu na yeye,” amesema Mnunka.