Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo Mbeya City arejea akiiwaza Singida Black Stars

KADER Pict

Muktasari:

  • Nyota huyo aliyetua kikosini humo msimu huu kutokea Fountain Gate, amecheza michezo mitano kati ya 10 ya Mbeya City kufuatia majeraha ya nyama za paja yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda.

BAADA ya kurejea uwanjani, kiungo wa Mbeya City, Ismail Aziz Kader, amesema anaenda kuanza upya ligi, huku akionesha kuumizwa na matokeo ya kipigo cha mabao 4-0 dhidi ya Azam, akiifungia kazi Singida Black Stars.

Nyota huyo aliyetua kikosini humo msimu huu kutokea Fountain Gate, amecheza michezo mitano kati ya 10 ya Mbeya City kufuatia majeraha ya nyama za paja yaliyomuweka nje ya uwanja kwa muda.

Straika huyo alikuwa na kiwango bora msimu uliopita akiisaidia Fountain Gate kumaliza salama Ligi Kuu, huku akifunga mabao matano na kusaidia matano kwa msimu mzima.

KADE 01

Hadi sasa hajafunga bao lolote akihusika kwenye moja ‘asisti’ na kufanya presha kuwa kubwa kikosini kuanzia vita ya namba na kuisaidia timu kuwa nafasi nzuri.

Pia Mbeya City iliyokuwa na mwanzo mzuri, imeonekana kukata pumzi ikishuka hadi nafasi ya 11 kwa pointi 10 baada ya kucheza mechi tisa na Novemba 2, 2026 itakuwa Sokoine jijini Mbeya kuikaribisha Singida Black Stars.

KADE 03

Akizungumza na Mwanaspoti, kiungo huyo amesema hawakufurahishwa na matokeo ya mchezo dhidi ya Azam, akieleza kuwa kwa sasa akili na nguvu zote zipo kwenye mechi ijayo dhidi ya Singida Black Stars kuhakikisha wanafanya kweli.

Amesema baada ya kukosekana uwanjani kwa muda kadhaa, sasa kazi inaenda kuanza upya akiahidi kurejesha kasi yake ya msimu uliopita kuisaidia timu hiyo na mwenyewe kujiweka katika ramani nzuri ya soka.

KADE 2

“Nashukuru nimerejea uwanjani baada ya kutoonekana kwa muda, hatuko pazuri sana lakini hatujakata tamaa na tunaweza kubadilika na kufanya vizuri, kimsingi ni kuendelea kupambana.

“Ni matokeo tu ya mpira lakini tunajipanga na mchezo ujao tutasahihisha makosa yaliyoonekana ili tuweze kushinda na kujitoa nafasi za chini, tuna ari, nguvu na hamasa kubwa,” amesema.