Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kiungo ataja tofauti ligi ya Misri, Tanzania

ARAFAT Pict

Muktasari:

  • Huu ni msimu wa pili mfululizo wa kiungo huyo kuitumikia timu hiyo akijiunga nayo msimu wa 2025/26 akitokea Namungo alipokuwa kwa mkopo kutoka Azam FC.

KIUNGO mshambuliaji wa Enppi SC inayoshiriki Ligi Kuu Misri, Arafat Ally amesema tofauti kubwa aliyogundua kati ya soka la Misri na Tanzania ni namna walivyowekeza na kuweka mfumo mzuri wa kuendeleza vipaji vya vijana.

Nahodha huyo aliyeiongoza Timu ya taifa ya vijana U-20 kufuzu AFCON U-20 amesema Misri kuna ligi maalum na rasmi ya vijana, ambayo imekuwa ikiwajenga wachezaji tangu wakiwa wadogo na kuwatayarisha kwa ajili ya ushindani wa soka la kulipwa kabla ya kupandishwa katika vikosi vya wakubwa.

Alifafanua katika klabu 20 zinazoshiriki ligi hiyo, kila mmoja inatakiwa kuwa na timu yake ya vijana, jambo linalorahisisha mchakato wa kuandaa nyota wa baadaye.

Arafat alieleza mfumo huo mzuri na unaofuatiliwa kwa karibu ndiyo siri inayofanya wachezaji wengi wa Misri kupata fursa za kujiunga na klabu kubwa Ulaya na duniani.

"Ndiyo maana wenzetu wachezaji wengi ni rahisi kuuzika nje hata Ulaya kwa sababu wana mfumo mzuri wa ligi ya vijana na unaofuatiliwa," amesema kiungo huyo

"Hapa kwetu naona pia hilo limeanza kuonekana na naamini likiendelea na kuboreshwa zaidi na kusapotiwa kwa ukubwa, itakuwa moja ya ligi shindani sana za vijana."

Huu ni msimu wa pili mfululizo wa kiungo huyo kuitumikia timu hiyo akijiunga nayo msimu wa 2025/26 akitokea Namungo alipokuwa kwa mkopo kutoka Azam FC.