Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Joseph Jr: Kucheza Hispania siyo rahisi

JOSE Pict

Muktasari:

  • Usajili wa beki huyo katika klabu hiyo ulikamilika mapema mwaka huu kupitia timu ya vijana (Juvenil B), hatua inayotajwa kuwa mwanzo mzuri katika taaluma yake ya soka.

BEKI Mtanzania, Joseph Junior Michael anayekipiga katika timu ya vijana ya Juvenil B, U19 inayomilikiwa na klabu ya Celta Vigo ya Hispania, amesema kucheza kwenye ligi ya División de Honor Juvenil sio rahisi hata kidogo kutokana na ushindani ulivyo.

Joseph, ambaye anacheza nafasi ya beki wa kati, ameweka wazi ingawa maisha ya soka Hispania yana ushindani mkubwa, anatumia kila fursa anayopata kujifunza vitu vipya kutoka kwa nyota wenye uzoefu klabuni hapo.

"Hispania siyo rahisi lakini napambana sana kwa nafasi niliyopewa. Najifunza sana kutoka kwa wachezaji wengi huku," amesema Joseph.

Mbali na maisha ya klabu, beki huyo kijana alitoa shukrani kwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya vijana ya Tanzania (Ngorongoro Heroes), Mario Rivera Campesino ambaye alimpa nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya vijana U-20 mechi za kufuzu AFCON U-20.

Joseph alikuwa mmoja wa wachezaji waliopata nafasi ya kuanza na kuonyesha kiwango kwenye mechi dhidi ya dhidi ya Ethiopia na Ngorongoro Heroes ilishinda mabao 4-0.

Akishuhudia hatua za mwanaye, baba mzazi wa beki huyo, Jose Mara amesema kupata nafasi Celta Vigo U19 si mchezo na kuongeza: "Kijana wangu kupata nafasi kwenye kikosi cha Celta Vigo U19 haikuwa rahisi kutokana na nafasi chache zinazopatikana kwenye kituo hicho. Tangu acheze Hispania kuna vitu vimebadilika kwa kijana wangu, hasa kutoka kwenye soka la kufundishwa hadi lile la Ulaya."

Safari ya soka ya Joseph ilianzia Tanzania katika akademi ya Magnet Youth Sports na uwezo na kipaji chake vilionekana mapema kabla ya kwenda Ulaya.

Usajili wa beki huyo katika klabu hiyo ulikamilika mapema mwaka huu kupitia timu ya vijana (Juvenil B), hatua inayotajwa kuwa mwanzo mzuri katika taaluma yake ya soka.