Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kisa Morrison... Nabi afoka

YANGA kuna mastaa watatu mpaka sasa hawajaripoti kambini ambao ni winga Bernard Morrison, kiungo Stephane Aziz KI na beki Yannick Bangala na kabla hawajajiunga na timu hiyo kuna mkwara mzito wametumiwa na kocha wao Nasreddine Nabi na hakuishia hapo akatua pia kwa mashabiki wa timu hiyo.
Nabi amekuwa mbogo akisema katika kila timu anayofundisha staa pekee ni klabu na sio yeye wala mchezaji yoyote na kwamba hakuna ambaye atamsumbua kwa nidhamu kisha akabaki salama, akionyesha kukerwa na wanachofanya mastaa hao.
Nabi alisema amechukizwa na kuchelewa kujiunga na timu hiyo kwa mastaa wao na kwamba timu haiwezi kuendeshwa kwa ruhusa za mara kwa mara, bila kuzingatia muda wa kurejea kwa wakati.
Juzi mashabiki pamoja na kwamba timu yao ilishinda walikuwa walikuwa wakihoji sana kuhusu walipo mastaa wao kadhaa ambao hawakuonekana uwanjani au kwenye benchi la timu yao wakati ikivaana na Ihefu.
"Sina tatizo na mchezaji kuomba ruhusa, hata mimi kama kocha huwa naomba ruhusa lakini unaheshimu muda wa kurejea kazini, siwezi kuwa na furaha na mchezaji ambaye hana heshima na klabu, hakuna staa mkubwa kuliko hii timu,"alisema Nabi.
"Nilisema wakati nafika hapa mara ya kwanza, mimi siyo kocha wa kuishi kwa furaha na mchezaji aliyeshindwa kufuata misingi ya nidhamu, naweza nisikupange ukaa benchi nikawapa nafasi wengine wanaoheshimu klabu hii," alisema kocha huyo ambaye msimu huu wa ligi amepoteza mchezo mmoja tu.
Mbali na wachezaji Nabi aliwatumia salamu pia mashabiki wa Yanga akisema wakati atakapoanza kuchukua hatua hizo asitoee yeyote akahoji kwanini mchezaji fulani hapewi nafasi wakati wanaona hana nidhamu.
"Huwa nakutana na maswali kwamba kwanini mchezaji fulani hapewi nafasi, nitakapoanza kuchukua hatua kali sitajibu swali la namna hiyo, nafikiri hili linapaswa pia kuzingatiwa na mashabiki, tuko hapa Yanga kwa ajili ya kazi na siyo mambo mengine ya nje ya hapo.
Pamoja na kwamba, kocha huyo hakuwataja wachezaji hao moja kwa moja, lakini Mwanaspoti linafahamu kuwa alikuwa akiwazungumzia, Morisson, Bangala na Aziz Ki ambao walipewa ruhusu na hadi juzi kwenye mchezo dhidi ya Ihefu hawakuwepo uwanjani.
Morrison alikuwa staa wa kwanza Yanga kuondoka nchini kabla ya ligi kusimama Desemba akiukosa hata mchezo wa mwisho mwaka jana dhidi ya Mtibwa Sugar akiwa bado hajarejea huku wenzake Bangala na Aziz Ki wakiondoka baadaye baada ya ligi kusimama na hadi juzi wakati wa mechi hiyo hakuwapo.