Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Wembe afichua jambo

KIPa Pict

Muktasari:

  • Wembe ilivuna pointi hizo baada ya kutoka sare dhidi ya Raskazone na Muembe Makumbi City, matokeo ambayo Njiku amesema hayakuwiana na kiwango walichoonyesha uwanjani.

KIPA wa Wembe, Victor Marceline Njiku amesema walistahili kuondoka na alama sita katika mechi zao mbili za ugenini kisiwani Unguja, lakini matumizi mabaya ya nafasi yaliifanya kurejea nyumbani na pointi mbili pekee.

Wembe ilivuna pointi hizo baada ya kutoka sare dhidi ya Raskazone na Muembe Makumbi City, matokeo ambayo Njiku amesema hayakuwiana na kiwango walichoonyesha uwanjani.

Njiku amesema katika michezo yote miwili, Wembe ilitengeneza nafasi nyingi za kufunga kuliko wapinzani wake, lakini wachezaji walishindwa kuzitumia vizuri na kuzigeuza kuwa mabao.

Amesema matokeo hayo yamekwenda tofauti na mipango waliyojiwekea kabla ya safari hiyo, ingawa bado wanashukuru kwa kupata pointi mbili kutokana na ugumu na ushindani mkubwa wa ligi.

“Wembe, mikakati yetu ni kuondoka na alama katika kila mchezo. Kama si alama tatu, basi angalau moja, kwa sababu lengo letu ni kumaliza ligi katika nafasi nzuri,” amesema Njiku.

Kipa huyo amesema sasa timu hiyo inarejea nyumbani kwa ajili ya kujiandaa na michezo mitano iliyobaki kabla ya kukamilika kwa mzunguko wa kwanza wa ligi.

Wembe inatarajiwa kucheza dhidi ya KMKM, Mafunzo, Polisi, KVZ na Chipukizi United katika michezo yake mitano iliyosalia.

Njiku amesema kila mchezo uliobaki utakuwa muhimu kwa Wembe, hivyo kikosi hicho kinahitaji kuongeza umakini na kuhakikisha kinatumia vizuri nafasi kitakazotengeneza ili kutimiza malengo yake ya kumaliza msimu katika nafasi nzuri.