Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Nne zilizopanda daraja hali mbaya ZPL

DARAJA Pict

Muktasari:

  • Msimamo wa ligi hiyo kabla ya mechi ya jana, unaongozwa na Zimamoto yenye pointi 22, Polisi ikiwa ya pili na pointi 21, huku JKU ikiwa ya tatu na pointi 17.

TIMU nne zilizopanda daraja msimu huu ikiwemo Black Sailors, Wembe, Raskazone na Mwenge, bado hazijaanza vizuri katika Ligi Kuu Zanzibar (ZPL).

Kati ya timu hizo, mbili zimebadilisha mabenchi ya ufundi kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya ambazo ni Wembe na Mwenge.

Mwenge katika mechi tisa ilizocheza, imeshinda moja, sare tatu na kupoteza tano na kukusanya pointi sita ikiwa nafasi ya 15 katika msimamo wa Ligi Kuu.

Mbali na Mwenge, Black Sailors nayo ipo kwenye hali mbaya ikiwa nafasi ya 13 ya msimamo wa ligi hiyo ikikusanya pointi tisa kati ya mechi tisa ilizocheza, imeshinda michezo miwili, sare tatu na kupoteza nne.

Timu ya Wembe ambayo imecheza mechi kumi, ipo nafasi ya kumi katika msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 11 sawa na ilizonazo Raskazone iliyopo nafasi ya 11.

Katika mechi ambazo imecheza Wembe, imeshinda mbili, sare tano na kupoteza tatu huku Raskazone ikishinda michezo mitatu, sare mbili na kupoteza tano.

Msimamo wa ligi hiyo kabla ya mechi ya jana, unaongozwa na Zimamoto yenye pointi 22, Polisi ikiwa ya pili na pointi 21, huku JKU ikiwa ya tatu na pointi 17.