Farid Mzalendo apewe nafasi Ligi Kuu
Muktasari:
- Ingekuwa ni amri yetu hapa kijiweni, yule dogo tungempeleka kwa mkopo katika timu mojawapo inayoshiriki Ligi Kuu ili apate nafasi ya kucheza na kukomaa kiushindani zaidi kuliko kutumika katika kikosi cha vijana tu.
AZAM FC wana yule dogo wana yule dogo anaitwa Farid Mzalendo wa kikosi chao cha vijana, anajua sana mpira yule.
Ni winga wa kisasa ambaye anaweza kuwa na mchango mkubwa kwa timu anayoichezea iwe Azam au tofauti na wauza aiskrimu hao wa kule Chamazi.
Sasa kijiwe kikiangalia ile busta ya mawinga iliyopo pale Azam ya wakubwa na mahitaji ya matokeo ambayo ile timu inayo kwenye ligi na mashindano mengine, kinaona itakuwa ngumu sana kwa Mzalendo kupenya kikosi cha kwanza msimu huu.
Ingekuwa ni amri yetu hapa kijiweni, yule dogo tungempeleka kwa mkopo katika timu mojawapo inayoshiriki Ligi Kuu ili apate nafasi ya kucheza na kukomaa kiushindani zaidi kuliko kutumika katika kikosi cha vijana tu.
Kuna timu nyingi tu za Ligi Kuu ambazo yule mtoto anaweza kuzichezea na akazisaidia zifanye vizuri kwenye mechi zao kuliko hata baadhi ya wachezaji ambao wamo kwenye vikosi vyao hivi sasa.
Kwanza ana uwezo wa kupunguza mabeki kwa chenga, kutengeneza nafasi na kufunga na pia ana kasi huku akiwa mnyumbulifu sasa mchezaji mwenye sifa kama hizo ni muhimu katika ligi yetu hii.
Dirisha dogo la usajili linakuja timu zimchangamkie yule Farid Mziwanda na zimuombe kwa mkopo na kijiwe kinaamini wale Azam FC hawawezi kumuwekea kauzibe yule bwana mdogo.
Si mnakumbuka Novatus Dismas walimtoa kwa mkopo Biashara United akawaka hadi wakamuuza Ulaya wakapata mihela ya kutosha.