Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kipa Simba avunja ukimya

Muktasari:

  • Nyota huyo amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti aliyopata tangu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) iliyofanyika Morocco mwaka 2025, akiwa katika maandalizi na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

KIPA wa Simba, Yakoub Suleiman Ali, amesema licha ya kukaa nje ya uwanja kwa sasa, lakini anafurahishwa na maendeleo ya timu hiyo kiujumla, huku akiwapongeza wachezaji wote wa kikosi hicho kutokana na kuendelea kupambana ili kufikia malengo yao.

Nyota huyo amekuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu akiuguza majeraha ya goti aliyopata tangu Fainali za Kombe la Mataifa Afrika (AFCON) iliyofanyika Morocco mwaka 2025, akiwa katika maandalizi na kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Akizungumza na Mwanaspoti, Yakoub alisema kukaa nje kwa muda mrefu ni jambo linalomuumiza kwa sasa kwa sababu malengo ni kuipambania timu itwae mataji mbalimbali inayopigania, japo kiwango cha wachezaji wenzake kinampa pia matumaini makubwa.

“Kila mchezaji anatamani kuipambania timu kufikia malengo iliyojiwekea, kwangu imekuwa tofauti kwa sasa kwa sababu niko nje ya majukumu yangu, ila ninafurahia wenzangu wanavyozidi kupambana katika kila mechi tunazozicheza,” alisema Yakoub.

Akizungumzia ushindani wake na kipa mwenzake, Mahamadou Tanja Kassali, Yakoub alisema kukaa nje kwa muda mrefu ni moja ya changamoto anayopitia ili akirejea aendelee kuaminika na benchi la ufundi, japo anapenda anachoendelea kukionyesha.

“Kwa sasa nimefikia asilimia 50 ya matibabu ninayopata na ikifika Desemba 2026, au kabla ya hapo kuna uwezekano nikaanza kurejea uwanjani, nashukuru uongozi wa Simba, mashabiki zangu kwa kuendelea kuniombea kwa kipindi hiki,” alisema Yakoub.

Mara ya mwisho Yakoub kucheza ilikuwa ni kichapo cha Simba cha mabao 2-0 dhidi ya Azam FC katika Ligi Kuu, Desemba 7, 2025 kwenye Uwanja wa Mkapa.