Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kilichomkuta Changarawe 'Sauzi' kimemfunza mengi

CHANGALAWE Pict

Muktasari:

  • Changarawe, ambaye aliwahi kuwa bondia kabla ya kuingia kwenye ukocha, alisema tofauti na zamani ambapo wengi walijihusisha na ngumi kwa mazoea na kujifurahisha, kwa sasa mchezo huo umegeuka kuwa njia ya kujipatia kipato na kujenga maisha.

MWENYEKITI wa Kamati ya Ufundi na Utafiti ya Shirikisho la Ngumi Kitaifa, Meja Mstaafu Michael Changarawe, amesema ngumi zimebadilika na sasa ni ajira inayoweza kumuingizia kipato kijana, akiwataka mabondia kuitumia fursa hiyo kuwekeza kwenye mchezo huo.

Changarawe, ambaye aliwahi kuwa bondia kabla ya kuingia kwenye ukocha, alisema tofauti na zamani ambapo wengi walijihusisha na ngumi kwa mazoea na kujifurahisha, kwa sasa mchezo huo umegeuka kuwa njia ya kujipatia kipato na kujenga maisha.

Changarawe alianza kucheza ngumi mwaka 1973 na kuhitimisha safari yake ya ulingoni mwaka 1988, kabla ya kuanza rasmi kazi ya ukocha mwaka 1989. Katika kujiimarisha kitaaluma, alipata Astashahada ya ukocha wa ngumi nchini Zambia, Cheti cha Ngazi ya Juu nchini Ujerumani na Diploma nchini Hungary.

Akizungumza na Mwanaspoti, mkongwe huyo alisema anaendelea kutumia uzoefu na elimu yake kuandaa mabondia, licha ya kukabiliwa na changamoto mbalimbali zinazofanya kazi yake isiwe na manufaa makubwa ya kiuchumi kama ambavyo anatamani itokee.

Alisema katika kipindi chote alichokuwa akifundisha, amefanikiwa kuzalisha mabondia zaidi ya 100, lakini jambo linalomuumiza ni kwamba, licha ya mchango huo katika maendeleo ya mchezo nchini, bado anakabiliwa na changamoto za maisha ya kila siku, ikiwemo usafiri.

CHANGA 01

“Yaani kwa mabondia niliowafundisha, nikipata hata bajaji ya kusafiria itakuwa imenisaidia angalau kidogo, kwa sababu kwa uzee niliofikia, mambo ya usafiri si rahisi hususani daladala nikipata inaweza kuniingizia walau kipato cha kila siku kuliko kutegemea watoto,” alisema Changarawe.

Akiwa na umri wa miaka 76, Changarawe hajakata tamaa ya kufundisha ngumi akitoa maarifa  kwa vijana wanaotaka kujenga majina yao kupitia mchezo huo, ingawa anakiri kazi hiyo haijamletea kipato cha kutosha kulingana na mahitaji yake.

Miongoni mwa mabondia waliopitia mikononi mwake ni nahodha wa timu ya taifa ya Tanzania, Yusuph Changarawe anayejulikana pia kama Yusuf Changarawe. Bondia huyo ni mtoto wa mdogo wake Changarawe mwingine ni Mashaka Malulu, ambaye anajihusisha na ngumi za kulipwa nchini Marekani na wengineo.

Changarawe anaamini safari yake ni ushahidi wa namna mchezo wa ngumi unavyoweza kuibua vipaji na kuandaa mabondia wa ngazi ya taifa. Hata hivyo, simulizi yake inaibua pia mjadala kuhusu namna ya kuwatambua na kuwawezesha makocha wakongwe ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa kukuza vipaji, ili waendelee kutoa huduma zao huku wakipata maisha.