Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo Pamba Jiji aingilia kati

KIGOGO Pict

Muktasari:

  • Pamba Jiji ndiyo inaburuza mkia kwa pointi moja baada ya kucheza mechi sita, hali ambayo imeonekana kuwavuruga mashabiki na uongozi katika kukwepa aibu ya kushuka daraja.

WAKATI mashabiki na wadau wa soka jijini Mwanza wakifura juu ya matokeo yasiyoridhisha kwa Pamba Jiji, uongozi wa timu hiyo umeibuka na kukiri kutokuwa na mwanzo mzuri, huku ukitaja sababu na hatma yao msimu huu.

Pamba Jiji ndiyo inaburuza mkia kwa pointi moja baada ya kucheza mechi sita, hali ambayo imeonekana kuwavuruga mashabiki na uongozi katika kukwepa aibu ya kushuka daraja.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa timu hiyo, Peter Lehhet amekiri matokeo kutokuwa mazuri na nafasi waliyopo haiendani na hadhi, ukubwa wala heshima ya Pamba Jiji, hata hivyo, safari bado ni ndefu.

Amesema kutokana na hali hiyo zipo sababu zilizofanya hali hiyo ikiwa ni ratiba ngumu waliyoanza nayo kwa mechi tatu mfululizo zikihusisha vigogo wa soka nchini, Simba, Yanga na Azam kisha kukutana na JKT Tanzania.

PAMBA 01

“Lakini tumepata majeruhi ya nyota wetu akiwamo beki Bryan Ishehanda na Shasiri Nahimana na kipa Stephen Ochieng ambao vibali vyao vilikuwa bado, tunaamini hadi mechi ijayo dhidi ya Geita Gold itakuwa tayari.

“Uongozi umechukua hatua za kiutawala na kifundi kurejesha utulivu, niwaombe mashabiki wote kuweka kando tofauti zetu na badala yake tuendelee kushirikiana na kutoa hamasa uwanjani” amesema Lahhet.

Kigogo huyo ameongeza, bado wanayo nafasi kubwa ya kusahihisha na kurekebisha, kwa kuwa msimu uliopita na wa sasa, utofauti wake ni pointi mbili kwa takwimu kwa mechi sita.

PAMBA 02

Alikiri yapo baadhi ya mapungufu ikiwamo makosa binafsi ya wachezaji, akitolea mfano mechi iliyopita dhidi ya TRA United walipopoteza 3-1 na benchi la ufundi litafanyia kazi.

“Msimu uliopita katika mechi sita tulivuna pointi tatu kati ya 18, msimu huu pointi moja, mapungufu yaliyopo ni eneo la straika ambapo kocha Francis Baraza anapaswa kulifanyia kazi na tumemwambia,” amesema ofisa huyo.

Hata hivyo bosi huyo aliwahakikishia wadau na mashabiki wa soka jijini humo kuwa licha ya matokeo hayo, lakini hawapo nyuma sana na badala yake wanaweza kurudi kwa kishindo na timu kurejesha ari, nguvu na morali mpya.