Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kigogo Bigman aitaka Ligi Kuu

KIGOGO Pict

Muktasari:

  • Safari hii, mabosi wa timu hiyo wanasema liwake jua, inyeshe mvua, msimu huu hawataki kusikia chochote zaidi ya kutimiza lengo la kupanda daraja.

BAADA ya kushindwa kutimiza ndoto ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2026/27 kutokana na kufanya vibaya kwenye Ligi ya Championship msimu uliopita, Bigman FC imetangaza vita mpya.

Safari hii, mabosi wa timu hiyo wanasema liwake jua, inyeshe mvua, msimu huu hawataki kusikia chochote zaidi ya kutimiza lengo la kupanda daraja.

Bigman imeingia kwenye msimu mpya ikiwa na matumaini makubwa baada ya kufanya usajili wa wachezaji wenye majina, uzoefu na uwezo wa kucheza soka la ushindani.

Timu hiyo iliyokuwa ikifahamika kama Mwadui FC ya Shinyanga kabla ya kuuzwa, kubadilishwa jina na kuhamishiwa Tanga, msimu uliopita ilimaliza Championship ikiwa nafasi ya 11 kwa pointi 36.

KIGO 01

Lakini sasa imefanya marekebisho na kuanza ukurasa mpya, huku lengo likiwa moja ni kupanda Ligi Kuu Bara.

Mkurugenzi wa Bigman FC, Ahamed Waziri amesema maandalizi ya msimu mpya yameanza mapema ili kuhakikisha timu hiyo haijirudii makosa ya msimu uliopita.

Waziri amesema lengo lao ni kuona Bigman inafanya vizuri kwenye Championship na hatimaye kupata tiketi ya kucheza Ligi Kuu.

Amesema kwa sasa timu ipo kambini kisiwani Pemba kwa ajili ya maandalizi, kabla ya kurejea Tanga kuendelea na programu rasmi ya kujiandaa na msimu mpya.

KIGO 02

“Tunayo matarajio makubwa kutokana na mipango tuliyonayo. Msimu uliopita haukuwa mzuri kwa sababu hatukufikia malengo yetu. Kwa sasa tumesafisha na kuboresha kikosi ili kutimiza ndoto yetu,” amesema Waziri.

Waziri alitamba kwamba Bigman imefanya usajili wa wachezaji wenye uwezo na uzoefu mkubwa katika soka la ushindani, akiamini uwepo wao utakuwa silaha muhimu katika mbio za kupanda daraja.

“Tunao wachezaji bora wenye majina makubwa na wanaofanya vizuri kwenye soka la ushindani, akiwemo Steven Say, kipa Nurudin Barola, Geofrey Mwashiuya na Peter Albogast ‘Shalulile’,” amesema.

Naye kocha Mkuu wa Bigman, Amanzi Nurdin amesema kuaminiwa kupewa jukumu la kuiongoza timu hiyo ni nafasi anayotaka kuitumia kuandika historia mpya.

KIGO 03

Nurdin anaamini msimu ujao unaweza kuwa wa neema kwake kwa kuipandisha Bigman Ligi Kuu, huku akitaja ushirikiano uliopo ndani ya timu kuwa moja ya silaha kubwa.

“Kwanza tunahitaji maandalizi mazuri ndani ya uwanja na kuwaweka vijana sawa kisaikolojia, kwa sababu tunao wachezaji wenye uzoefu wa ligi. Matarajio yangu ni kuona tunafanya kweli msimu ujao,” amesema.

Kocha huyo pia amejieleza kuwa ana uzoefu wa kutosha katika soka la ushindani, kutokana na historia yake ya kucheza ndani na nje ya Tanzania.

“Nina uwezo na uzoefu wa ligi za ushindani. Nimecheza Majimaji, Njombe Mji na Ruvu Shooting, lakini hata nje ya nchi nimecheza Aigle Noir ya Burundi na Karonga United ya Malawi. Pia nimeibua mastaa wengi ambao sasa wanafanya vizuri Ligi Kuu,” amesema.