Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

KIBAMBA: Zoezi la kuchukua fomu Simba linaenda vizuri

Muktasari:

  • TFF kupitia kamati ya uchaguzi ya Shirikisho hilo iliamua kusimamia uchaguzi huo baada ya kuonekana kuna pande mbili zinasigana kuhusiana na uchaguzi huo.

MWENYEKITI wa Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wakili Kiomoni Kibamba, amesema utaratibu wa uchukuaji wa fomu kwa wanaotaka kugombea uongozi Simba unakwenda vizuri.

TFF kupitia kamati ya uchaguzi ya Shirikisho hilo iliamua kusimamia uchaguzi huo baada ya kuonekana kuna pande mbili zinasigana kuhusiana na uchaguzi huo.

"Hadi sasa zoezi la kuchukua fomu linaendelea vizuri, kila kitu kinaenda sawa, hilo ndilo ninaloweza kuzungumza kwa sasa," amesema.

Zoezi la uchukuaji wa fomu lilianza rasmi jana Novemba 16, 2026, baadhi yao waliokuwa wamechukua ni Geofrey Nyange Kaburu anayewania nafasi ya mwenyekiti, Christopher Mwansasu ujumbe wa bodi ya wakurugenzi katika klabu hiyo.

Leo Novemba 17, 2026 Agness Daniel Maarufu 'Aggy Simba' amechukua fomu ya kugombea ujumbe wa klabu hiyo na zoezi hilo la uchukuaji fomu linaendelea.

Kibamba, alitangaza uchaguzi huo kufanyika Januari 30, badala ya Januari 3, 2027, ili viongozi watakaopatikana watapokea kijiti cha viongozi wanaomaliza muda wao chini ya mwenyekiti,Murtaza Ally Mangungu.


BAADHI YA MATUKIO YA LEO

Watu waliokuwa wamevalia jezi za Simba,walifika nje ya geti la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakiwa wamebeba mabango yenye jumbe mbalimbali, huku wakisikika wakisema wanataka haki yao.

Pamoja na watu hao kuimba nyimbo zao huku wakipiga ngoma, walinzi wa getini hawakuwafungulia geti, baada ya muda waliondoka.

Zilipita takribani dakika 45 baada ya watu hao kuondoka, gari la polisi likafika katika eneo hilo na kukuta watu hao wameshaondoka.