Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kete ya mwisho WPL leo, matokeo kuamua bingwa

Muktasari:

  • Katika kuhitimisha msimu, michezo miwili ambayo Gets Program dhidi JKT Queens na Alliance Girls dhidi Simba Queens, itaenda kuamua bingwa wa ligi hiyo kutokana na msimamo ulivyo.

MZUNGUKO wa mwisho wa Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) msimu wa 2024-2025 unahitimishwa leo Mei 20, 2025 kwa mechi tano kuchezwa huku Mlandizi Queens na Gets Program zikiwa tayari zimeshuka daraja.

Katika kuhitimisha msimu, michezo miwili ambayo Gets Program dhidi JKT Queens na Alliance Girls dhidi Simba Queens, itaenda kuamua bingwa wa ligi hiyo kutokana na msimamo ulivyo.

JKT Queens na Simba Queens zimelingana pointi kwenye msimamo zote zikiwa na 44 baada ya kucheza mechi 17 zikitofautiana mabao ya kufunga na kufungwa.

Ili Simba Queens itetee ubingwa wa ligi hiyo, inatakiwa kushinda dhidi ya Alliance Girls huku ikiombea JKT Queens ipoteze au kutoka sare dhidi ya Gets Program.

JKT Queens inausaka ubingwa wa ligi hiyo ilioupoteza msimu uliopita huku ikifukuzia rekodi ya Simba Queens inayoongoza kubeba mara nne. Kwa sasa JKT Queens imeshinda ubingwa huo mara tatu.

Rekodi za mabingwa wa Ligi Kuu Wanawake zinaonyesha hivi; Mlandizi Queens (2017), JKT Queens (2017/2018), JKT Queens (2018/2019), Simba Queens (2019/2020), Simba Queens (2020/2021), Simba Queens (2021/2022), JKT Queens (2022/2023) na Simba Queens (2023/2024).


MECHI ZA MWISHO WPL

Alliance Girls πŸ†š Simba Queens

πŸ•“ Saa 10 Jioni

🏟️ TFF Center Kigamboni


Gets Program πŸ†š JKT Queens

πŸ•“ Saa 10 Jioni

🏟️ Jamhuri Stadium Dodoma


Yanga Princess πŸ†š Ceasiaa Queens

πŸ•“ Saa 10 Jioni

🏟️ KMC Complex


Mashujaa Queens πŸ†š Bunda Queens

πŸ•“ Saa 10 Jioni

🏟️ TRA Mivinjeni Dar


Fountain Princess πŸ†š Mlandizi Queens

πŸ•“ Saa 10 Jioni

🏟️ Tanzanite Kwaraa