Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kauli ya kwanza ya Manara baada ya kutemwa Simba

Aliyekuwa Msemaji wa Simba, Haji Manara amefunguka kwa mara ya kwanza baada ya uongozi wa timu hiyo kutoa taarifa ya kuachana nae leo Julai 28, 2021.

Nafasi ya Manara imezibwa na mwanahabari Ezekiel Kamwaga ambaye atakaimu kwa miezi miwili.

Kupitia mtandao wa Instagram, Manara ameweka picha akiwa ameshika begi akitembea na kuandika neno kubwa kwake ni Alhamdulillah akimaanisha anamshukuru Mungu.

Ameandika; "Kila tunapomaliza Mechi yoyote ile ya Simba, neno langu la kwanza baada ya matokeo yoyote yale ni Alhamdulillah.
Kwa wanaofuatilia page hii wanatambua hilo. Kwangu neno hili ndio Msamiati nnauotumia mara nyingi zaidi na hufanya hv kwa kila jambo ,liwe jema au baya. Yes neno langu ni moja tu
 AL-HAMDULILLAH"