Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kapilima ajiweka kando Bigman FC

KAPILIMA Pict

Muktasari:

  • Katika mechi sita ilizocheza Bigman FC, imeanza vibaya msimu huu baada ya kupoteza tano na kutoa sare moja, ikiwa mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi yake moja tu, huku safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ikifunga mabao matano na kuruhusu 13.

MZIMU wa makocha umeendelea kukitesa kikosi cha Bigman FC cha jijini, Tanga, baada ya aliyekuwa kocha mkuu wa timu hiyo, Omary Kapilima kuachia ngazi, huku akiweka wazi sababu kubwa iliyomfanya aondoke ni matokeo mabaya inayoendelea kupata.

Akizungumza na Mwanaspoti, kocha huyo wa zamani wa KenGold FC ya jijini Mbeya, amesema ameamua kuachana na kikosi hicho kwa masilahi mapana, licha ya wachezaji na mashabiki wa timu hiyo kumuonyeshea sapoti ya kutosha tangu alipojiunga nayo.

"Ni mapema sana ila nimeamua kuondoka ili kuachia wengine waendeleze pale nilipoishia, zipo sababu nyingi lakini kwangu matokeo yasiyoridhisha ni miongoni pia, nawashukuru kwa ushirikiano walionipa tangu nilipojiunga nao," amesema Kapilima.

Kapilima aliyewahi kufundisha na kucheza timu mbalimbali zikiwemo za Majimaji, Yanga na Mtibwa Sugar, amekuwa ni kocha wa pili msimu huu wa 2026-2027, kuachana na Bigman FC zamani Mwadui FC, baada ya mwanzoni kuondoka kwa Amanzi Nurdin.

Katika mechi sita ilizocheza Bigman FC, imeanza vibaya msimu huu baada ya kupoteza tano na kutoa sare moja, ikiwa mkiani mwa nafasi ya 16 na pointi yake moja tu, huku safu ya ushambuliaji ya kikosi hicho ikifunga mabao matano na kuruhusu 13.