Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kajumulo amvaa Tenga TFF,Leodegar Tenga

Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

MWANDISHI WETU BAADA ya kupotea kwa muda mrefu, mdau wa soka Alex Kajumulo ameibuka kuwania nafasi ya Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF). Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) umepangwa kufanyika Febuari 24, mwaka huu. Kajumulo ambaye alitingisha soka la Tanzania katika miaka ya 1999, anakuwa mtu wa pili kutaka nafasi hiyo baada ya Jamal Malinzi, ambaye alishatangaza nia mapema. "Nimeamua kujitosa kuwania nafasi hii kwa kuamini nina sifa ya kuongoza soka letu kutokana na mengi niliyowahi kufanya huko nyuma," alisema Kajumulo. Rais wa TFF, Leodegar Tenga, bado hajaweka wazi kama anagombea ingawa habari za ndani zinasema ameamua kuwania kwa awamu ya tatu. Kajumulo alivuma katika soka la Tanzania mwaka 1997 wakati alipoichukua timu ya Sigara kutoka kwa mdau wa soka kuibadili jina kuwa Kajumulo World Soccer. Katika taarifa yake, Kajumulo alisema anajivunia kuanzisha klabu ya kulipwa na ndio mtu wa kwanza kupeleka timu Brazil. Mwanaspoti linafahamu kuwa jambo hilo si la kweli kwani Kajumulo si timu ya kwanza ya Tanzania kwenda Brazil. Yanga ndiyo iliyokuwa timu ya kwanza Tanzania kwenda huko mwaka 1974, Pan African ilikuwa ya pili mwaka 1979 na Simba mwaka 1982. Kajumulo alieleza pia yeye ndiye aliyewasaidia nyota wa zamani kama Nteze Johm, Kally Ongala, Salvatory Edward na John Mwansasu kwenda kucheza soka nje ya Tanzania.