Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Kabaddi yaanza vibaya Jumuiya ya Madola

KABADI Pict

Muktasari:

  • Katika mechi za kwanza, Tanzania ndio timu iliyofunga pointi chache zaidi ambazo ni 21, huku Austalia ikifunga pointi nyingi 59.

TIMU ya Taifa ya Kabaddi ya wanaume kutoka Tanzania, imeanza vibaya kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola yanayoendelea nchini India baada ya kufungwa pointi 48-21 na SRI Lanka.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Abass khamis Suleiman, amesema wameanza kupoteza mchezo wa kwanza katika mashindano hayo kwa sababu ya presha waliyokuwa nayo wachezaji.

Mbali na hilo, kocha huyo amesema wachezaji wao hawana viatu maalumu vya kuchezea mchezo huo ambavyo huchangia kwa kiasi kikubwa kuwapa balansi uwanjani.

“Kupoteza mchezo wa kwanza kuna vitu ambavyo vilisababisha ikiwemo wachezaji kuwa na presha kubwa ya mchezo pamoja na kukosa viatu vya kuchezea Kabaddi ambavyo vinasaidia kuwa na balansi nzuri uwanjani,” amesema.

Hata hivyo, amesema timu bado haijapoteza muelekeo wa mashindano hayo, hivyo wanajiandaa kufanya vizuri katika mechi zijazo kwa lengo la kumaliza wakiwa katika nafasi nzuri na kuliheshimisha Taifa.

Katika mchezo mwingine, Timu ya Taifa ya Kenya imeibuka na ushindi wa kuifunga Singapore pointi 48-28, huku Australia ikipokea kibano cha kufungwa pointi 59-30 kutoka kwa Scotland.

Wakati huohuo, wenyeji wa mashindano hayo, Timu ya Taifa ya India imeibuka na ushindi wa pointi 46-26 dhidi ya England, huku Uganda ikiifunga Malaysia pointi 45-29.

Katika mechi za kwanza, Tanzania ndio timu iliyofunga pointi chache zaidi ambazo ni 21, huku Austalia ikifunga pointi nyingi 59.