Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mlandege yamkalia kooni Msomali

MLANDEGE Pict

Muktasari:

  • Taarifa iliyotolewa na timu hiyo, ilieleza uongozi wa Mlandege umeamua kuchukua hatua hiyo ili Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ifuatilie mwenendo wa mwamuzi huyo aliyechezesha mechi hiyo ya Septemba 23, 2026.

MLANDEGE imeiomba Bodi ya Ligi Zanzibar (ZBL) kumchukulia hatua mwamuzi wa kati, Nassor Salum 'Msomali' kwa kile ilichokidai hakuzingatia sheria 17 za mpira wa miguu kwenye mechi yao dhidi ya KVZ.

Taarifa iliyotolewa na timu hiyo, ilieleza uongozi wa Mlandege umeamua kuchukua hatua hiyo ili Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji wa Ligi ifuatilie mwenendo wa mwamuzi huyo aliyechezesha mechi hiyo ya Septemba 23, 2026.

Mlandege iliyopoteza mechi hiyo kwa mabao 2-0, inadai mwamuzi huyo hakuwa mwadilifu wala kuzisimamia sheria za mpira kama inavyotakiwa kwa kuwanyima pigo la penati kwa makusudi.

"Vitendo alivyovifanya ni vingi ikiwemo mchezaji wa KVZ kumkanyaga kwa makusudi mchezaji wetu na kutunyima pigo la panalti ilihali vilifanyika wazi na wengi tumeshuhudia," ilieleza taarifa hiyo.

Kutokana na hilo, Mlandege ilisema imeondoa imani kwa mwamuzi huyo na kuomba asipangwe kwenye mechi zinazoihusu huku uongozi ukihitaji achukuliwe hatua za kinidhamu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Katibu Mkuu wa Mlandege, Hussein Ahmada alithibitisha wameandika barua kwa Ofisa Mtendaji Mkuu wa Bodi, Issa Kassim Ali kwa lengo la Mwamuzi huyo kuchukuliwa hatua.

"Hiyo barua tumeiandikia Bodi ya Ligi Zanzibar, hivyo tunasubiria majibu kutoka kwao," amesema Ahmada.