Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Mohamed Shilla ataka kuivunja rekodi yake Sweden

SHILLA Pict

Muktasari:

  • Shilla alikuwa na muendelezo mzuri tangu akiwa U-17 msimu wa 2023/24 alifunga mabao 15 akiibuka MVP wa ligi hiyo. Msimu uliofuata alifunga mabao 12 na asisti tano kwenye mechi 22.

NYOTA wa AIK inayoshiriki Ligi Kuu ya Sweden, Mohamed Shilla amesema malengo yake msimu huu ni kuifikia na kuivuka rekodi yake ya mabao 12 na asisti saba ya msimu uliopita 2025/26.

Akizungumza na Mwanaspoti, Shilla ambaye alimaliza msimu uliopita akiwa na kiwango bora kilichomfanya azidi kuaminiwa na benchi la ufundi la timu hiyo, amesema mafanikio hayo yamempa hamasa ya kufanya vizuri zaidi na malengo aliyojiwekea ni ya kuvunja rekodi hiyo.

“Kuanza vizuri kunakupa mwanzo mzuri wa kutoka sehemu moja kwenda nyingine, kwa sababu unapokuwa chini ukipanda juu unakutana na upinzani unaokufanya ukue,” amesema Shilla.

“Siyo rahisi, lakini naamini rekodi hiyo ya mabao nitaivunja. Unajua ni ngumu, ila mimi huwa napenda kujitathmini mwenyewe na kujiwekea malengo,” anasema.

Mbali na kufunga mabao, Shilla anaona msimu huu kama fursa ya kuendelea kujenga uzoefu na kuonyesha kiwango alichokionyesha msimu uliopita haikuwa bahati.

Akiwa Azam kinda huyo mwenye miaka 18 alimaliza msimu wa 2025/26 akiwa mchezaji bora wa ligi ya vijana na Azam FC ilikuwa bingwa wa mashindano ya U-20 akifunga mabao manane na asisti tano kwenye mechi 14.

Shilla alikuwa na muendelezo mzuri tangu akiwa U-17 msimu wa 2023/24 alifunga mabao 15 akiibuka MVP wa ligi hiyo. Msimu uliofuata alifunga mabao 12 na asisti tano kwenye mechi 22.