Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Jengo la Yanga Kariakoo kugharimu Sh5.5 bilioni

Muktasari:

  • Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, amesema ujenzi wa Yanga Tower unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja, ikiwa ni sehemu ya mipango ya klabu hiyo kuongeza vyanzo vya mapato na kujiimarisha kiuchumi.

YANGA SC, imeanza rasmi safari ya kujenga jengo la kisasa la Yanga Tower, baada ya uongozi wa klabu hiyo kusaini mkataba na kampuni ya Group 6 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi huo wenye thamani ya Sh5.5 bilioni.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Septemba 9, 2026 jijini Dar es Salaam katika hafla ya utiaji saini wa mkataba huo, Rais wa Yanga, Mhandisi Hersi Said, amesema ujenzi wa Yanga Tower unatarajiwa kukamilika ndani ya mwaka mmoja, ikiwa ni sehemu ya mipango ya klabu hiyo kuongeza vyanzo vya mapato na kujiimarisha kiuchumi.

Hersi amesema jengo hilo lililopo Mtaa wa Mafia na Nyamwezi, Kariakoo jijini Dar es Salaam, litakuwa na jumla ya ghorofa 14, huku ghorofa tatu za chini zikitengwa kwa ajili ya shughuli za biashara, wakati sehemu nyingine za juu zitatumika kwa ajili ya makazi. Mpangilio huo unalenga kuhakikisha jengo hilo linakuwa mali yenye uwezo wa kuingizia klabu mapato ya muda mrefu.

“Mradi utakuwa wa mwaka mmoja na itakuwa ghorofa 14. Tatu za chini zitakuwa za biashara na nyingine za juu zitakuwa za makazi. Mradi huu utakuwa wa Sh5.5 bilioni,” amesema Hersi.

Kwa mujibu wa Hersi, ujenzi wa Yanga Tower ni sehemu ya mpango mpana wa klabu hiyo wa kuwekeza katika miundombinu yake, huku akieleza kuwa mradi huo utaenda sambamba na ujenzi wa Uwanja wa Yanga unaotarajiwa kujengwa eneo la Jangwani.

Rais huyo amesema jengo hilo lilitolewa kwa Yanga mwaka 1964 na kwa kipindi kirefu lilikuwa likitumika kama makazi ya watu mbalimbali.

Hata hivyo, viongozi wa klabu walipokuja kutambua thamani ya kibiashara ya eneo hilo, wakaona kuna umuhimu wa kulibadilisha matumizi na kujenga jengo litakaloweza kuingizia Yanga mapato.