Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge azitaja mechi saba Azam

IBENGE Pict

Muktasari:

  • Azam ilianza ligi kwa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania iliyopanda daraja, lakini iliporudi nyumbani ikashinda mechi ngumu dhidi ya TRA United kwa mabao 2-1, kwenye mechi ambayo matajiri hao wa Chamazi walimaliza wakiwa pungufu mchezaji mmoja kufuatia kipa Aishi Manula kuonyeshwa kadi nyekundu.

MASHABIKI wa Azam ni kama wana wasiwasi hivi juu ya kiwango cha timu hiyo mpaka sasa, lakini kocha wa kikosi hicho, Florent Ibenge amewashusha presha huku akisema wanahitaji kama mechi saba hivi ili kukaa sawa na kucheza kwa kiwango bora zaidi.

Azam ilianza ligi kwa sare ya bao 1-1 ugenini dhidi ya Polisi Tanzania iliyopanda daraja, lakini iliporudi nyumbani ikashinda mechi ngumu dhidi ya TRA United kwa mabao 2-1, kwenye mechi ambayo matajiri hao wa Chamazi walimaliza wakiwa pungufu mchezaji mmoja kufuatia kipa Aishi Manula kuonyeshwa kadi nyekundu.

Akizungumza na Mwanaspoti, Ibenge amesema bado timu yake haijafanikiwa kucheza kwa kiwango ambacho wanakitaka kutokana na wachezaji kuendelea kutafuta muunganiko unaotokana na wale wachezaji wapya na wengine waliosalia.

Ibenge amesema hatua ya kupata ushindi kwenye mchezo uliopita, ilikuwa muhimu kutokana na kujenga hali ya kujiamini ambapo wanahitaji angalau mechi saba ili kuweza kuwa sawasawa.

IBENG 01

“Hatukupata muda wa kutosha sana kwenye maandalizi yetu ya mwanzo wa msimu, lakini hatulalamiki kitu ambacho tunatakiwa kukifanya haraka ni kutafuta muunganiko wa wachezaji tuliowaongeza na wale ambao walibaki hapa,” amesema Ibenge.

"Kuna wachezaji wapya wameanza kuonyesha wanaweza kuzoea kwa haraka, lakini wapo wengine ambao walisalia nao wameonyesha ni uti wa mgongo wa timu.

IBENG 02

“Nafahamu mashabiki wanahitaji Azam iliyo bora, kila kitu kinawezekana tuna timu bora lakini tunahitaji mechi kama saba hivi ili tuweze kucheza kwa ubora ambao tunatamani kuwa nao, jambo zuri tumerudi kwenye njia ya kushinda."

IBENG 03
IBENG 03

Azam jana ilikuwa uwanjani kucheza mechi yake ya tatu ya Ligi Kuu Bara ikiwa mwenyeji wa Pamba Jiji kutoka Mwanza. Mechi hiyo ilipigwa Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.