Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Ibenge aomba radhi, Azam ikianza vibaya Shirikisho

RADHI Pict

Muktasari:

  • Kocha huyo amekiri kuwa hawakupata matokeo waliyokuwa wanayahitaji licha ya maandalizi waliyofanya na jitihada za wachezaji wake ndani ya uwanja.

KOCHA wa Azam FC, Florent Ibenge, ameomba radhi kwa mashabiki wa timu hiyo baada ya kikosi chake kupoteza kwa mabao 2-1 dhidi ya Al Ahly Tripoli ya Libya, akisema matokeo hayo yamewaumiza kwa sababu walikuwa na nafasi ya kuibuka na ushindi.

Ibenge amesema Azam ilifanya vizuri katika baadhi ya vipindi vya mchezo huo, ikatengeneza nafasi za kufunga, lakini tatizo kubwa lilikuwa kushindwa kuzitumia na kuruhusu wapinzani wao kuibuka na ushindi huo.

Kocha huyo amekiri kuwa hawakupata matokeo waliyokuwa wanayahitaji licha ya maandalizi waliyofanya na jitihada za wachezaji wake ndani ya uwanja.

AZA 01

“Ningependa kwanza kuomba radhi. Tulipata nafasi kadhaa na tulikuwa na uwezekano wa kushinda mchezo huu, lakini hatukuweza kuzitumia. Tumeumizwa na matokeo haya,” amesema Ibenge.

Akizungumzia hali ya kikosi chake, Ibenge pia amefichua changamoto ya majeraha, akieleza kuwa mmoja wa wachezaji wake, Himid Mao alipata maumivu wakati wa mazoezi na hali hiyo iliendelea hadi siku ya mchezo.

AZA 02

Hata hivyo, kocha huyo amesisitiza kuwa hawapaswi kukaa muda mrefu wakifikiria kipigo hicho, bali wanatakiwa kujipanga upya, kurekebisha makosa na kuelekeza nguvu zao katika mchezo unaofuata.

Ibenge amesema katika soka ushindi na kushindwa ni sehemu ya mchezo, hivyo muhimu kwa Azam ni kubaki pamoja, kujifunza kutokana na matokeo hayo na kuhakikisha wanarejea kwenye ushindani wakiwa bora zaidi.