Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Huyo Balama ndo basi tena!

Balama ndo basi tena

Muktasari:

  • KIUNGO machachari wa Yanga, Mapinduzi Balama ni kama ameonyeshewa mlango wa kutokea kutokana na kupotezewa kimtindo baada ya kupewa matibabu ya kutosha.

KIUNGO machachari wa Yanga, Mapinduzi Balama ni kama ameonyeshewa mlango wa kutokea kutokana na kupotezewa kimtindo baada ya kupewa matibabu ya kutosha.

Balama baada ya kufanyiwa upasuaji wa mguu wake, mabosi wa Yanga waliamua kumpa jezi yake namba saba mchezaji wao mpya Fiston Abdulrazack.

Kitendo cha mchezaji huyo kuchukua jezi ya Balama kinaonyesha kabisa kwamba Balama hana kilichobaki Yanga.

Cha kusikitisha zaidi msimu huu ndio mwisho wa mkataba wake baada ya yeye kusaini mkataba wa miaka miwili akitokea Alliance na ameichezea Yanga msimu mmoja tu.

Ni ngumu kuwashawishi mabosi wa Yanga kumpa mkataba mwingine, hata kama akibaki anakuwa pia kapoteza namba yake mgongoni mbele ya Fiston.