Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hiki hapa kilichomuondoa Ettiene TRA

Muktasari:

  • Ettiene raia wa Burundi alijiunga na timu hiyo tangu msimu uliopita baada ya timu hiyo kucheza mechi tatu za Ligi Kuu msimu wa 2025/26, bila kuwa na kocha mkuu, ambapo alionesha mafanikio kumaliza msimu nafasi ya tano kwa pointi 43.

MATOKEO yasiyoridhisha kwa TRA United yametajwa kuwa sababu za timu hiyo kufikia makubaliano ya pande zote na aliyekuwa Kocha Mkuu wake, Ettiene Ndayragije kuachana, huku uongozi ukihaha kusaka mbadala.

Ettiene raia wa Burundi alijiunga na timu hiyo tangu msimu uliopita baada ya timu hiyo kucheza mechi tatu za Ligi Kuu msimu wa 2025/26, bila kuwa na kocha mkuu, ambapo alionesha mafanikio kumaliza msimu nafasi ya tano kwa pointi 43.

Msimu huu hali imeonekana kuwa ngumu kwa Ettiene baada ya kuiongoza mechi tano akiambulia pointi tatu ikiwa ni sare tatu na kupoteza michezo miwili na kuwa nafasi ya 13 kwenye msimamo.

Ettiene mwenye uzoefu wa Ligi Kuu Bara anakumbukwa kwa kazi nzuri tangu alipotambulishwa nchini katika kikosi cha Mbao FC aliyoifikisha fainali ya Kombe la Shirikisho (kwa sasa CRDB), KMC, Azam na timu ya Taifa, Taifa Stars.

Ofisa Habari wa TRA United, Christina Mwagala ameliambia Mwanaspoti kuwa kwa faida ya timu, wameamua kuchukua hatua ya awali ya kuachana na kocha huyo kwa lengo la kurejesha heshima kutokana na matokeo waliyoanza nayo.

Amesema wakati wakiachana na Mrundi huyo, uongozi unaendelea kutafakari kwa ajili ya kumtafuta kocha mpya ambaye ataungana na ‘Wakusanya Kodi’ hao kwa lengo la kuendelea alipoishia mtangulizi wake.

“Hii ndio uamuzi wa awali kwa mustakabali wa timu, matokeo yamekuwa si mazuri kwetu hivyo kujua nani atakuja kusimamia benchi tusubiri wakati uongozi ukiendelea na mchakato huo na kutafakari nani anafaa kwa sasa”

“Tunatarajia TRA United itarejea upya katika Ligi Kuu baada ya kutokuwa na mwanzo mzuri, hatujakata tamaa na tunaamini kuanzia mchezo ujao dhidi ya Pamba Jiji tutafanya vizuri,” amesema Mwagala.