Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hesabu nyingine kwa Yanga Ligi Kuu Bara

YANGA Pict

Muktasari:

  • Yanga inaingia uwanjani ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu ya mwanzo, hivyo ushindi mwingine utaiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kutawala ligi mapema.

BAADA ya kuanza kwa kishindo, Mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga leo Ijumaa itakuwa na kazi ya kuhakikisha inaendelea kukaa kileleni mwa msimamo wa ligi, itakapokutana na Pamba Jiji katika mchezo unaotarajiwa kuchezwa kwenye Uwanja wa KMC Complex, Dar es Salaam kuanzia saa 3:00 usiku.

Yanga inaingia uwanjani ikiwa na pointi tisa baada ya kushinda michezo yote mitatu ya mwanzo, hivyo ushindi mwingine utaiweka katika nafasi nzuri ya kuendelea kutawala ligi mapema.

Pamba Jiji kwa upande wake ina kiu kubwa ya kuandika ushindi wake wa kwanza msimu huu baada ya kuanza kwa sare ya 1-1 dhidi ya Dodoma Jiji, kabla ya kufungwa 2-1 na Simba, kisha kupoteza kwa matokeo kama hayo dhidi ya Azam FC.

YANG 01

Yanga inataka kuendelea kuwa kileleni, wakati Pamba Jiji inatafuta ushindi ambao unaweza kuwa mwanzo wa kuibadilisha safari yake katika msimu huu.

Tangu imerejea Ligi Kuu Bara msimu wa 2024-2025, Pamba Jiji imekutana na Yanga mara mbili, haijashinda zaidi ya kupokea vipigo vyote, huku mbaya zaidi, haijafunga bao.

Yanga katika mechi nne dhidi ya Pamba Jiji, imefunga mabao 13 bila ya nyavu zake kutikiswa. Msimu wa 2024-2025, Yanga iliifunga Pamba Jiji jumla ya mabao 7-0 katika mechi mbili, kisha 2025-2026 ikashinda jumla ya mabao 6-0 mechi mbili.

Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi, amekiri kuwa maandalizi ya mchezo huo yamekuwa na muda mfupi kutokana na ratiba kubana, lakini amesema hilo haliwezi kuwa kisingizio.

“Kusema ukweli nitakuwa nadanganya kama nitasema tumepata muda wa kutosha kujiandaa na mchezo huu, kwani ni siku tatu tu tangu tucheze mechi yetu iliyopita. Lakini hii si kisingizio kwa sababu hata mpinzani wetu, Kocha Baraza, anakabiliwa na changamoto hiyo hiyo ya kubanwa kwa ratiba,” amesema Mngqithi.

YANG 02

Mngqithi pia ametoa taarifa kuhusu hali ya kikosi chake, akisema Clement Mzize anaendelea vizuri baada ya kutoka kwenye majeraha na anaweza kurejea uwanjani ndani ya mwezi mmoja kutoka sasa.

Kuhusu Stephane Aziz Ki, kocha huyo amesema mchezaji huyo bado hajawa tayari kwa asilimia 100 baada ya kukosa maandalizi ya msimu, akifichua kuwa kiwango chake cha utimamu wa mwili kwa sasa ni 4/10.

Hata hivyo, amesema klabu inamlinda kwa karibu ili kuepusha uwezekano wa kupata majeraha.

Kwa upande wa Pamba Jiji, Kocha Francis Baraza, amesema maandalizi yamekamilika na vijana wake wako tayari kwa vita hiyo.

Baraza amesema kikosi chake kimefanya mazoezi kwenye viwanja vya nyasi bandia na asilia, huku akisisitiza falsafa yake kwa wachezaji kwamba, mechi kubwa cheza kikubwa.

Amesema Pamba Jiji inaiheshimu Yanga lakini haiogopi, huku akifichua kuwa amefanya uchambuzi wa namna timu hiyo inavyocheza, hasa matumizi ya maeneo ya pembeni.

Kwa mujibu wa Baraza, Yanga imekuwa ikitengeneza hatari kubwa kupitia krosi kutoka pembeni, jambo ambalo amesema kikosi chake kitalilinda kwa umakini mkubwa.

YANG 03

“Tunaiheshimu Yanga, lakini hatuwaogopi hata kidogo. Nimefanya uchambuzi wa falsafa ya mwalimu wao na tunajua wako imara sana maeneo ya pembeni ambako wamekuwa wakifunga magoli mengi kutokana na krosi zao, hivyo tutajitahidi kuzuia milango yao yote na kupunguza makosa.

“Siku zote huwa nawaambia wachezaji wangu kuwa mechi kubwa cheza kikubwa, kiakili wako tayari na wanautaka sana mchezo huu baada ya sisi kuanza na mechi ngumu dhidi ya Simba na Azam,” amesema Baraza.

YANG 05

MBEYA CITY VS FOUNTAIN GATE

Mapema saa 10:00 jioni, Mbeya City itakuwa mwenyeji wa Fountain Gate kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya. Mbeya City yenye pointi sita, inalenga kuendeleza ushindi baada ya mechi ya kwanza kupoteza nyumbani dhidi ya Geita, kisha kuzifunga Dodoma Jiji (2-0) na Mashujaa (2-1).

Fountain Gate yenyewe itakuwa ikisaka ushindi wa pili baada ya kuanza kwa kusuasua ikifungwa 3-0 na Singida Black Stars, ikashinda 1-0 mbele ya Mashujaa, kisha ikapoteza 1-0 kwa Namungo. Rekodi zinaonyesha mechi nne za Ligi Kuu Bara baina ya timu hizo, Fountain Gate imeshinda mbili, wakati Mbeya City imeshinda moja. Sare moja.

YANG 04

GEITA GOLD VS AZAM

Saa 12:30 jioni kwenye Uwanja wa Bukombe mkoani Geita, wenyeji Geita Gold wataikaribisha Azam.

Geita Gold ikiwa na pointi sita ilizokusanya kwa kuzifunga Mbeya City (1-0) na Kagera Sugar (6-2), huku ikifungwa na Namungo (1-0), inakutana na Azam yenye pointi saba ikianza na sare ya 1-1 dhidi ya Polisi Tanzania, ikaja kuzifunga TRA United na Pamba Jiji kwa matokeo ya 2-1.

Mara ya mwisho Mei 28, 2024, Azam iliichapa Geita Gold 2-0 ikiwa ugenini, kati ya mechi sita walizokutana  katika ligi Azam imeshinda tatu na sare tatu.