Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Manqoba agusia nafasi ya Aziz KI, Mwalimu Yanga

Muktasari:

  • Yanga ilifanya usajili wa dakika za jioni kwa kumshusha kiungo Aziz KI na kumnyakua Mwalimu anayecheza ushambuliaji kutoka mikononi mwa wapinzani wake wakubwa, Simba.

UKIWAULIZA mashabiki wa Yanga wanashauku ya kuwaona mastaa gani uwanjani, basi watamtaja Stephanie Aziz KI na Seleman Mwalimu ambao mpaka sasa hawajawaona dimbani, huku sajili zao zikitikisa anga.

Yanga ilifanya usajili wa dakika za jioni kwa kumshusha kiungo Aziz KI na kumnyakua Mwalimu anayecheza ushambuliaji kutoka mikononi mwa wapinzani wake wakubwa, Simba.

Mastaa hawa wote walisajiliwa kutoka kwenye timu za Afrika Kaskazini. Aziz KI akitokea Ittihad ya Libya na Mwalimu akitokea timu aliyowahi kuichezea Mburkinabe huyo, Wydad Casablanca ya Morocco.

Mwalimu alimaliza msimu wa 2025-2026 akiwa na Simba na kuacha rekodi ya kufunga mabao tisa ya Ligi Kuu Bara, huku Aziz KI akiichezea Yanga kwa misimu mitatu na kufunga jumla ya mabao 52.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kocha wa Yanga, Manqoba Mngqithi amesema mastaa hao wataanza kuonekana uwanjani wakati wowote kuanzia sasa kwa sababu walihitaji muda zaidi.

"Seleman Mwalimu au kiungo Stephanie Aziz KI hakuna sababu nyingine zaidi ya kutofikia hatua ninayoitaka hasa ya ufiti wa mwili ndio maana huwaoni kwenye mechi kama hivi.

"Lakini wanaendelea kuimarishwa na wakati wowote wataonekana kwenye mechi ambazo timu itakwenda kucheza, kwa sababu huu ni mwanzo wa msimu sio mwisho, wakiwa tayari wataonekana," amesema kocha huyo.

Ameongeza kuwa, mpaka sasa kuna wachezaji ambao alianza nao maandalizi ya msimu huu (pre-season) lakini ndio wanaingia kwenye mfumo taratibu, hivyo walioko nje sio wawili tu.

"Kabla ya Mwalimu, wapo wachezaji ambao walikuja mapema lakini bado hawajaonekana, huku nao wakiendelea kuimarishwa akiwemo kiungo mkabaji Fred Ngoma na Juma Issa 'Chuga' ambaye ndio amecheza kwa mara ya kwanza."

Kwa upande wa Chuga ni kama msoto wa benchi unaanza kumtoka baada ya kucheza mechi ya kwanza Agosti 24, 2026 tangu atue Yanga msimu huu, akitokea benchi na kupewa dakika 26 kuchukua nafasi ya Albert Kangwanda.

Yanga mpaka sasa imecheza mechi tatu za Ligi Kuu Bara ikiwa haina rekodi ya kupoteza ikifunga mabao 11 na kuruhusu mawili dhidi ya Namungo na Coastal Union.