Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Hawa wanaweza wasirudi Bongo

BONGO Pict

Muktasari:

  • Mashindano makubwa kama haya hayaangaliwi na mashabiki tu wapo Makocha, mawakala na wawakilishi wa klabu mbalimbali ambao hufuatilia vipaji vinavyojitokeza, na kwa wachezaji vijana, dakika chache za kuonyesha uwezo zinaweza kuwa mwanzo wa hatua nyingine kwenye maisha yao ya soka.

TANZANIA haikuanza vizuri katika mechi yake ya kwanza ya Kombe la Dunia la Wanawake U-20 baada ya kupoteza kwa mabao 4-1 dhidi ya Brazil, lakini ndani ya matokeo hayo kuna wachezaji walioonyesha kiwango bora.

Mashindano makubwa kama haya hayaangaliwi na mashabiki tu wapo Makocha, mawakala na wawakilishi wa klabu mbalimbali ambao hufuatilia vipaji vinavyojitokeza, na kwa wachezaji vijana, dakika chache za kuonyesha uwezo zinaweza kuwa mwanzo wa hatua nyingine kwenye maisha yao ya soka.

Winfrida Gerald ni mmoja wa majina hayo. Winga huyo wa JKT Queens alifunga bao moja la Tanzania dhidi ya Brazil, akifunga kwa mkwaju wa penalti.

BONG 03

Achana na bao hilo lakini nyota huyo alikuwa mchezaji muhimu wa kuisaidia Tanzanite kufuzu kucheza mashindano hayo makubwa akifunga bao dhidi ya Cameroon.  Mwingine ni kiungo mshambuliaji wa Fountain Gate Princess, Mary Siyame ambaye yupo kwa mkopo Simba Queens, ni miongoni mwa wachezaji wenye uwezo wa kucheza mbele na katikati ya uwanja.

Jamila Rajabu, mshambuliaji kinda wa JKT Queens, ambaye amekuwa akipata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Twiga Stars, licha ya kwamba hakufunga bao kwenye Kombe la Dunia lakini uwezo wake wa kuwatoka mabeki na kusogea kwenye eneo la mpinzani ni mimoja ya silaha zake.

BONG 02

Ester Maseke, beki wa kati wa JKT Queens, naye ni mmoja wa wachezaji wa kuangaliwa. Katika mechi dhidi ya Brazil aliishinda mipira mitatu ya juu ya hatari licha ya Tanzania kuelemewa.

Hivyo kwa viwango vya wachezaji hao wanaweza kuwa moja ya wachezaji watakaojiuza kupitia mashindano hayo hata kama timu haitafanya vizuri.