Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Harusi ya Okwi imenogaje!!!a

Mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi na mkewe Florence Nakalega wakipata picha ya pamoja katika harusi yao iliyofungwa juzi Jumamosi nchini Uganda.

Muktasari:

  • Harusi yake imegharimu Dola 80,000 za Kimarekani ambayo ni sawa na Sh160milioni za Kitanzania.
  • Okwi amwaga chozi alipokuwa akieleza wasifu wa mke wake
  • Hamisi Kiiza apata kazi ya usimamizi

JUZI Jumamosi Jiji la Kampala lilisimama kwa muda kutokana na shamrashamra zilizoanikiza harusi ya mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Okwi alipoamua kuikacha klabu ya ukapera kwa kufunga ndoa iliyoacha gumzo jijini humo.

Straika huyo aliyewahi kuzichezea pia timu za Etoile du Sahel ya Tunisia, SC Villa ya Uganda na Yanga ya Tanzania alifunga ndoa iliyoacha historia nchini hapa kutokana na jinsi ilivyopambwa na kufana vilivyo.

Harusi hiyo iliyohudhuriwa na mastaa mbalimbali nyota wa Uganda, inadaiwa kuteketeza kiasi cha Dola 80,000 ambao ni kama Sh160 milioni za Tanzania, kiasi ambacho kingetosha kabisa kukamilisha usajili wa timu zisizopungua tatu katika Ligi Kuu ya Tanzania Bara.

Gazeti la Mwanaspoti lililotimba Uganda na kushuhudia kila kitu kilivyokuwa kinaendelea katika harusi hiyo, ambayo Okwi amemuoa mrembo aitwaye Florence Nakalega ambaye pia ni Mganda.

Nyota wa zamani wa Yanga na Uganda the Cranes, Hamis Kiiza ‘Diego’ na Nabisubi Julian ndiyo waliokuwa wasimamizi wa wanandoa hao katika kiapo kilichofungwa katika Kanisa la Miracle Centre Cathedral lililopo Lubaga mjini Kampala.

Mara baada ya shughuli ya kupiga picha maharusi hao kwa ajili ya ukumbusho wa tukio hilo muhimu kwa mwanadamu, kazi ilienda kuanza upya kwenye hoteli kubwa ya kifahari ya Munyonyo Resort Beach na moto uliwashwa zaidi kwenye Ukumbi wa Main Exhibition Hall uliopo ndani ya jengo la UMA maeneo ya Lugogo.

 

NDOA

Katika kula kiapo cha ndoa, wanandoa hao walifungishwa ndoa yao kanisani na Mchungaji Kayanja na baada ya kuwa mume na mke, safari ya kwenda kwenye hoteli ya kifahari ya Munyonyo ilianza kwa ajili ya kwenda kupiga picha za ukumbusho.

Waliokwenda kushiriki tukio hilo muhimu walikuwa ni maharusi wenyewe, wasimamizi, wapambe wake na marafiki wachache wa karibu wa wanandoa hao.

Cha kustaajabisha ni kwamba, msafara ulikuwa na magari yasiyopungua 15, kati ya hayo, magari saba yalikuwa maalumu kwa ajili ya maharusi na wasimamizi wao.

Magari matano yalikuwa aina ya Jaguar na Okwi alipanda Jaguar na mawili yalikuwa Brevis. Huko hakukuwa na mambo mengi zaidi ya picha tu na baada ya hapo, msafara kwenda ukumbini ukaanza.

 

AJALI

Safari ya kutoka Munyonyo kwenda Lugogo kwenye ukumbi wa Main Exhibition ilianza salama, lakini kwa bahati mbaya msafara huo ukiwa njiani ulipata ajali.

Gari mbili zilizokuwa kwenye msafara huo, ziligongana zenyewe kwa zenyewe na tamu zaidi, zilifanyiwa marekebisho usiku huo huo zikawa safi na kuendelea kudunda kama kawaida.

Gari hizo ni zile zilizokuwa zimewabeba wasimamizi wa maharusi akiwamo Kiiza na lile la Waandishi wa Habari, akiwamo Mwandishi wa Mwanaspoti na japo hakuna mtu aliyekuwa amejeruhiwa, lakini ajali hiyo ilileta taharuki kubwa kwa wahusika wote.

Chanzo cha tukio hilo ni gari la kina Kiiza kufunga breki ghafla.

 

MAMBO UKUMBINI

Hapa ndipo palikuwa na utamu kamili wa sherehe za harusi hiyo, kwani maharusi waliingia ukumbini saa 11 jioni, Okwi na wapambe wake wakivalia suti za bluu na Bi Harusi kutinga Shela Jeupe.

Hata hivyo punde tu mambo yalikuwa mengine kwani watu walienda kubadilisha mavazi, wanaume walivaa suti za khaki wakati Bi harusi alivaa gauni lenye rangi ya kijivu.

Okwi alipokelewa na wachezaji wenzake waliokuwa wameshika mipira kwa juu na yeye akapita katikati yao huku wakicheza na baada ya hapo walikabidhiwa mpira na makocha Sam Simbwa na Moses Basena.

Baada ya hapo burudani, chakula, vinywaji na mambo mengine yakaendelea kwa kwenda mbele. Hakukuwa na pombe yoyote kwani familia ya Okwi ni walokole.

Keki ilipambwa kwa urembo mwingi na kuwa kivutio, huku jamaa wawili waliokuwa wamevalia kiasili ndiyo waliokuwa walinzi na kuongoza pia zoezi zima la kupiga fataki zilizohanikisha ukumbi huo kwa mwonekano wa rangi na sauti zilizosisimua.

 

WAMWAGA CHOZI

Katika hali isiyo ya kawaida na pengine kuonyesha furaha waliyokuwa nayo, Okwi alijikuta akidondosha chozi alipokuwa anazungumzia wasifu wa mkewe, Florence na kulia kabisa baada ya kuona chozi la mkewe ambaye ndiye aliyeanza kuelezea wasifu wa mumewe.

Lugha iliyokuwa ikitumika ukumbini hapo ni ya Luganda na yalitumika maneno machache ya Kiingereza, ili kunogesha zaidi.

Hata hivyo, Okwi alipoulizwa sababu ya kulia alifunguka na kudai: “Nililia kutokana na furaha kwani tumepita katika mzingira ya kila namna, magumu na raha.”

“Nimefurahi sana kukamilisha shughuli hii na sasa nina mke ambaye tutatengeneza familia moja na atakuwa mshauri wangu.”

 

MAMILIONI YATEKETEA

Waliosema kuwa starehe gharama hawakukosea kwani katika kupendezesha shughuli hiyo, haikuwa kirahisi hivi hivi tu, na badala yake kiasi kikubwa cha fedha kiliteketezwa kama utani.

Inaelezwa kuwa zaidi ya Dola za Kimarekani 80,000 ambazo ni kama Sh160 milioni, zilitumika kufanikisha mchongo mzima wa sherehe hizo.

Sehemu ya pesa hizo ni zile zilizotumika kwa gharama za ukumbi ambao ulikodishwa kwa pesa ya Uganda milioni 5 kwa Tanzania ni sawa na Sh3 milioni pamoja na mapambo, chakula, muziki, wasanii na mambo mengine.

Baadhi ya wasanii walioburudisha ni pamoja na Mchungaji Wilson Bugembe, Sophia Namtongo na Rehema.

 

MASTAA KIBAO

Mastaa waliofanikiwa kuhudhuria katika harusi hiyo ili kumuunga mkono Okwi ni pamoja na Rais wa Shirikisho la Soka la Uganda (Fufa), Moses Magogo na Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Uganda, Milutin ‘Micho’ Sredojevic Micho.

Wengine ni Makocha Moses Basena, Sam Simbwa na meneja wa The Cranes, huku upande wa wachezaji waliongozwa na nahodha wa Uganda, Andrew Mwesigwa aliyefuatana na mkewe, Dorine Nachintu na watoto wake, Cindy na Aarondy.

Pia walikuwamo Solomon Masaba, James Onyango, Robert Odonkara, Robert Ssentongo, Geofrey Sserunkuma, Gilbert Okelo, Henry Kiseka na Bwete, na kwa heshima walitambulishwa na Mwesigwa ndiye aliyetoa nasaha zake za busara kwa Okwi na mkewe Florence.