Halloween ya Soka: Mechi tano za kusisimua ukiwa na MELBET
Manchester United wanawatia hofu mashabiki wao, jijini Milan kutakuwa na pambano kati ya timu mbili ambazo bado hazijapoteza mchezo wowote kwenye ligi, huku Juventus wakijiandaa na keki ya kusherehekea miaka 129 tangu kuanzishwa kwa klabu hiyo.
Wikendi hii, tarehe 31 Oktoba na tarehe 1 Novemba, soka halihitaji mavazi yoyote ya Halloween ili kuleta msisimko.
MELBET inaangazia mechi tano kubwa zaidi za wikendi hii.
Chelsea dhidi ya Manchester United, Ligi Kuu ya Uingereza, tarehe 31 Oktoba
Manchester United hawajashinda mechi nane mfululizo, na walipoteza mchezo wao wa mwisho wa ligi kwa mabao 3-0 dhidi ya Bournemouth, huku Bruno Fernandes akikaa benchi kwa dakika zote za mchezo.
Je, walimuweka nje mchezaji wao muhimu wakiwa katika harakati za kutafuta mbinu mpya? Kuna jambo haliko sawa kwenye mpango huo, ingawa hata kiwango cha Bruno mwenyewe kimekuwa sio cha kuvutia sana.
Frank Ilett hajanyoa nywele tangu mwezi Oktoba 2024. Shabiki huyo anasubiri Mashetani Wekundu washinde mechi tano mfululizo, na katika kipindi hichi, nywele zake zimekua na kuwa ndefu kupita kiasi.
Kwa matokeo ya aina hii, hivi karibuni atahitaji viti viwili jukwaani: kimoja kwa ajili yake na kingine kwa ajili ya nywele zake. Michael Carrick yuko kwenye hatari ya kupoteza kazi yake kabla hata Frank hajafika kwa kinyozi.
Lakini Chelsea nao si wakamilifu: wamefunga mabao 17 na kuruhusu mabao 15 katika mechi nane. The Blues walipoteza kwa mabao ya 2-0 dhidi ya Tottenham. Jamani, tunazungumzia Tottenham hapa hata Manchester United waliweza kutoka sare nao.
Utabiri wetu: Chelsea kushinda kwa odds za 1.835.
Bayern Munich dhidi ya Borussia Dortmund, Ligi Kuu ya Ujerumani, tarehe 31 Oktoba.
Timu zote mbili zina pointi 17 baada ya kucheza mechi saba bila kupoteza. Bayern wamefunga mabao 25, wakati Borussia wamefunga mabao 12 pekee. Kikosi cha Niko Kovač kinajikusanyia pointi hasa kutokana na safu yake imara ya ulinzi, lakini itakuwa vigumu sana kuzuia mashambulizi ya Bayern.
Michael Olise amefunga mabao sita, huku Harry Kane akiwa na mabao manne na pasi nne za mabao. Ikiwa mabeki wa Borussia wataelekeza nguvu zao kumdhibiti mshindi wa tuzo ya Ballon d'Or, watampa Olise nafasi zaidi, na winga huyo wa Ufaransa ataitumia vizuri.
Borussia Dortmund, maarufu kama Weusi na Manjano, wameruhusu mabao manne pekee katika mechi saba, na sasa jukumu lao kubwa ni kuhakikisha hawaruhusu mabao yote hayo katika usiku mmoja jijini Munich.
Utabiri wetu: Bayern kushinda kwa odds za 1.35.
Milan dhidi ya Inter, Ligi Kuu ya Italia(Serie A), tarehe 31 Oktoba.
Milan na Inter ni miongoni mwa timu zinazoongoza ligi, lakini zinatumia mbinu tofauti kujipatia ushindi.
Katika mzunguko wa nane, Milan waliifunga Udinese kwa urahisi mabao 2-0, huku Inter wakipindua matokeo dhidi ya Fiorentina kwa kufunga mabao katika dakika za 91 na 97 na kushinda kwa 2-1. Mashabiki wa Nerazzurri (Inter) huenda wakahitaji kupewa kifaa cha kupima mapigo ya moyo pamoja na tiketi zao za kuingia uwanjani.
Marcus Thuram alifunga bao na kusababisha penalti iliyoamua matokeo ya mchezo huwezi kupoteza umakini hata kwa sekunde moja unapokabiliana na mshambuliaji wa aina hiyo.
Hata hivyo, kikosi cha Cristian Chivu kinaruhusu zaidi ya bao moja kwa kila mchezo, jambo linaloashiria kuwepo kwa nafasi za kufunga kwa Christian Pulisic na wenzake.
Tunatarajia dabi ya Milan, maarufu kama Derby della Madonnina, kumalizika kwa sare huku timu zote mbili zikifungana mabao:
Timu zote mbili kufunga mabao kwa odds za 1.52.
Juventus dhidi ya Napoli, Ligi Kuu ya Italia(Serie A), tarehe 1 Novemba
Juventus watakuwa wakisherehekea miaka 129 tangu kuanzishwa kwa klabu yao siku ya mechi, lakini Napoli wako tayari kuharibu sherehe hizo.
Ushindi wa Juventus wa mabao 2-0 dhidi ya Lecce ulikuwa wa kuridhisha, ingawa Luciano Spalletti hakufurahishwa na jinsi timu yake ilivyopunguza kasi baada ya mapumziko.
Wakati huohuo, Scott McTominay wa Napoli amerejea kwenye kiwango chake bora alifunga mabao mawili dhidi ya Roma. Mgeni wa aina hiyo anaweza hata kuishia kula keki yote ya sherehe peke yake!
Juventus wanaonekana kupewa nafasi kubwa ya kushinda wakiwa nyumbani, lakini Napoli hawana mpango wa kuwazawadia pointi tatu kama zawadi ya siku ya kuzaliwa.
Tunaamini wenyeji watashinda, lakini tunachagua utabiri wenye tahadhari zaidi: Juventus kutopoteza kwa odds za 1.235.
Liverpool dhidi ya Arsenal, Ligi Kuu ya Uingereza, tarehe 1 Novemba
Liverpool wameshinda mechi nne mfululizo katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na Ligi Kuu ya Uingereza. The Reds wanaupeleka mpira haraka ndani ya eneo la hatari, na Alexander Isak anajua vizuri cha kufanya baada ya hapo.
Mshambuliaji huyo wa Uswidi tayari amefunga mabao sita kwenye ligi, hivyo inaonekana mfumo wa uchezaji wa Andoni Iraola unamfaa vizuri.
Arsenal bila shaka watategemea mipira ya adhabu na kona. Ezri Konsa na Gabriel walifunga mabao dhidi ya Everton na kufanya matokeo kuwa 2-0. Mikel Arteta anaamini kwamba bao lao la kwanza kwenye Ligi Kuu ya Uingereza lililotokana na kona litarejesha imani ya wachezaji katika mbinu hii.
Liverpool wanapaswa kuepuka kuwapa Arsenal kona na mipira ya adhabu karibu na lango lao. Everton wamejifunza kwa njia ngumu kwamba mabeki wa Arsenal wanajua jinsi ya kufumania nyavu.
Hata hivyo, kikosi cha Iraola kiko kwenye kiwango kizuri, na Isak anaendelea kufunga mabao mara kwa mara. Wakati huohuo, timu hiyo ya London itamkosa Bukayo Saka kutokana na majeraha, hivyo tunaamini wenyeji wataweza kuwafunga mabingwa hao.
Utabiri wetu: Liverpool kushinda kwa odds za 3.09.
Hadi tarehe tarehe 31 Oktoba, jiunge na promosheni ya Mzunguko wa Bahati wa Halloween ndani ya MELBET, zungusha Gurudumu la Kichawi (Mystical Wheel) na ujinyakulie ?mikeka ya bure, mizunguko ya bure na pointi za bonasi. Pia utapata nafasi ya kujishindia iPhone 17 Pro Max zawadi inayosisimua zaidi kuliko peremende chache za Halloween.
Weka mikeka kwenye mechi kubwa, shiriki kwenye promosheni na ufanye Halloween hii kuwa ya kipekee na isiyosahaulika!