Haji Manara aiombea Simba
Muktasari:
- Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewaombea wachezaji wa klabu ya simba wapone na kuendelea na majukumu yao.
Baada ya kuahirishwa mchezo wa Ligi Kuu ya NBC kati ya Kagera Sugar na Simba uliokuwa uchezwe leo katika Uwanja wa Kaitaba Mkoani Kagera, kutokana na wachezaji 16 wa Simba kuonekana kuwa na dalili za mafua na kukohoa, Msemaji wa klabu ya Yanga Haji Manara amewaombea wachezaji wa klabu ya simba wapone na kuendelea na majukumu yao.
“Maradhi yanapowatokea wenzenu hata kama mna upinzani gani lazma uwaombee dua wapone haraka,,ili waweze kurudi kucheza tena...”
“nimeyanukuu maneno ya king Pele alipowaombea Wachezaji nyota wa Sweden walioumwa mafua ,kabla ya mechi ya fainali ya kombe la dunia baina ya Waswidish na Wabrazil World Cup ya 1958 kule Stockholm”.
“Na cc wadau wa Soka tunawaombea wachezaji wa Simba wapone haraka ili warejee uwanjani tena.
“Mimi siamini zile za ndani eti sijui mishahara sijui bonus ya kutoka sare na Yanga,,,naamini wenzetu wamepata maradhi na Insha'Allah watapona” ameandika Manara kupita Instagram yake