Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Gamondi ana dakika 180 za mtego, rekodi Al Merrikj zashtua

YANGA juzi asubuhi ilicheza mechi ya kirafiki ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya mwisho ikiwa jijini Dar es Salaam kabla ya keshokutwa kusafiri kwenda Kigali, Rwanda kwa mchezo wa kwanza wa raundi ya pili ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Merrikh ya Sudan, huku kocha mkuu wa timu hiyo, Miguel Gamondi akiwa na kazi ya kukwepa mtego wa dakika 180 mbele ya Wasudani hao.

Yanga itavaana na Al Merrikh kwenye Uwanja wa Kigali Pele (zamani Nyamirambo), katika mechi hiyo ya ugenini kabla ya kurudiana wiki moja baadaye na mshindi wa jumla kutinga makundi ya michuano ya msimu huu, hatua ambayo Yanga ilicheza mara ya mwisho miaka 25 iliyopita.

Timu hiyo iliweka rekodi mwaka 1998, ikiwa ya kwanza kutoka Tanzania kucheza hatua hiyo mara baada ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) kufanya mabadiliko ya michuano hiyo iliyokuwa ikifahamika kama Klabu Bingwa Afrika hadi mwaka 1997, japo ilimaliza kinyonge kundini.

Mechi ya Yanga na Al Merrikh itakayopigwa Jumamosi itakuwa ya tano kwa timu hizo kukutana kwenye michuano ya CAF, mbali na kuvaana kwao zaidi ya mara mbili kwenye michuano ya Klabu Bingwa kwa Nchi za Afrika Mashariki na Kati (Kagame Cup).

Rekodi zinaonyesha kuwa mara ya kwanza wa timu hizo kukutana ilikuwa ni 1973 kwenye raundi ya kwanza ya Klabu Bingwa (sasa Ligi ya Mabingwa Afrika) na Yanga kung’olewa kwa jumla ya mabao 3-2, ikifungwa nyumbani 2-1 na kutoka sare ya 1-1 ugenini kisha kukutana tena kwenye play-off ya Kombe la Shirikisho.

Timu hizo zilikutana kwenye michuano hiyo ya mwaka 2007, ambapo mchezo wa kwanza nyumbani Yanga ililazimishwa suluhu kabla ya kwenda kupasuka ugenini kwa mabao 2-0 na kutolewa, hivyo kocha Gamondi ana kazi ya kufanya ili kuuweka mtego huo kwa Wasudan kwa timu hiyo ushindi wa mara ya kwanza.

Rekodi zinaonyesha Yanga haijawahi kuifunga Al Merrikh hata kwenye michuano ya Kagame, kwani mwaka 1986 ilipoteza fainali kwa penalti 4-2 baada ya dakika za kawaida kuisha kwa sare ya 2-2 na mara ya mwisho zilipokutana tena kwenye michuano hiyo ilipofanyika nchini, timu hizo zilitoka tena sare ya 2-1.

Hivyo, Gamondi na jeshi lake ambalo jana asubuhi liligawa dozi nene kwa kuifumua Kiluvya United kwa mabao 6-0, lina kazi ya kuhakikisha wanauvunja mfupa wa muda mrefu mbele ya Wasudani, kwani hata msimu uliopita Yanga ilicheza na Al Hilal ya Sudan kwenye raundi ya kwanza na kung’olewa kwa jumla ya mabao 2-1, baasa ya sare ya 1-1 nyumbani na kulala ugenini kisha kuangukia kwenye play-off ya Shirikisho na kufika hadi fainali.

Hata hivyo, kasi iliyoanza nayo Yanga kwenye mechi za mashindano sita ilizocheza hadi sasa zikiwamo mbili za Ngao ya Jamii, mbili za Ligi Kuu na nyingine kama hizo za Ligi ya Mabingwa Afrika ikifunga jumla ya mabao 19 kupitia wachezaji tisa tofauti, imewapa matumaini makubwa wadau na mashabiki wa klabu hiyo.

Yanga iliianza mechi za mashindano kwa kuifunga Azam mabao 2-0 kisha kutoka suluhu na Simba katika mechi ya fainali ya Ngao na kupoteza kwa penalti 3-1, kisha ikacheza mechi ya Ligi kwa kugawa dozi ya 5-0 kwa KMC na JKT Tanzania, huku kwenye michuano ya CAF ilianza kuichapa Asas ya Djibouti kwa mabao 2-0 na ziliporudiana ikainyoosha kwa mabao 5-1 na kutinga raundi ya pili kwa jumla ya mabao 7-1.

Kocha huyo alikaririwa na Mwanaspoti akisema anajua mechi hiyo dhidi ya Al Merrikh sio rahisi, lakini alichaanza kuisoma mapema kupiotia michezo miwili ilipocheza na Oyo de Otoho ya Jamhuri ya Congo na kufuzu raundi hiyo ya pili kwa faida ya bao la ugenini baada ya sare ya 1-1 ugenini na suluhu ikiwa Kigali.

Baadhi ya mastaa wa Yanga wakiwamo manahodha, Bakar Mwamnyeto na msaidizi, Dickson Job  walisema wanajua wana mchezo mgumu Kigali, lakini lengo la kila mchezaji na klabu kwa ujumla ni kuona wanauzika mzimu wa miaka 25 kwa timu hiyo kutocheza makundi, hasa baada ya kufika fainali ya Shirikisho Afrika.

Yanga itarudiana na Al Merrikh katika mechi itakayopigwa Septemba 30 jijini Dar es Salaam na kama itakuwa imepata matokeo mazuri ya jumla itatinga makundi ikiwa ni mara ya kwanza tangu 1998.