Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Fabrizio Romano atambulisha jezi mpya za Yanga CAF

FABRIZIO Pict

Muktasari:

  • Romano, ambaye ni miongoni mwa waandishi wanaotambulika zaidi duniani katika masuala ya usajili wa wachezaji, ameshiriki katika tukio hilo la utambulisho wa jezi akizitoa katika kifungashio maalum na kuitoa moja baada ya nyingine.

YANGA SC leo Septemba 2, 2026 imetambulisha rasmi jezi zake zitakazotumia katika Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2026-2027, huku zoezi hilo likifanyika kwa namna ya kipekee baada ya kuongozwa na mwandishi maarufu wa habari za michezo kutoka Italia, Fabrizio Romano.

Romano, ambaye ni miongoni mwa waandishi wanaotambulika zaidi duniani katika masuala ya usajili wa wachezaji, ameshiriki katika tukio hilo la utambulisho wa jezi akizitoa katika kifungashio maalum na kuitoa moja baada ya nyingine.

Katika utambulisho huo, Romano ameanza kwa kusema: “Siku ya kufungua vifungashio (unboxing day) leo, washikaji. Haya basi, twende kazi.”

Akiendelea kuonyesha jezi hizo, Romano alionyesha kuvutiwa na muonekano wake huku akiisifia zaidi yenye rangi ya kijani.

"Oh, waoh, waoh, waoh! Tazama hii (jezi nyeusi). Inapendeza, eh? Pia ipo ya manjano. Inashangaza!
Kisha... ah, hii ndiyo bora zaidi! (jezi ya kijani)."

Kisha akahitimisha kwa kuitaja Yanga kama moja ya klabu kubwa Tanzania na Afrika Mashariki.

Katika maelezo yake, Romano amesema: “Young Africans Sports Club, klabu ya mpira wa miguu yenye mafanikio makubwa zaidi nchini Tanzania na Afrika Mashariki, inatambulisha jezi ya CAF Champions League ya msimu wa 2026-2027.”

Romano ameongeza kuwa, jezi hiyo imeandaliwa mahsusi kwa ajili ya safari ya Yanga katika mashindano ya juu ya klabu barani Afrika.

“Fahari ya Wananchi, iliyotengenezwa kwa ajili ya jukwaa la bara hili. Yanga, Bingwa!”

Utambulisho huo umeongeza mvuto katika maandalizi ya Yanga kuelekea kampeni yake ya Ligi ya Mabingwa Afrika msimu huu, huku jezi hiyo ikiwa sehemu ya utambulisho wa klabu katika jukwaa la kimataifa.

Kushirikishwa kwa Romano, anayefahamika zaidi duniani kwa taarifa zake za usajili kupitia mitandao ya kijamii na vyombo mbalimbali vya habari, kumeufanya uzinduzi huo kuwa wa aina yake na kuongeza mwonekano wa kimataifa kwa Yanga.

Yanga, ambayo ni moja ya klabu kongwe na zenye mafanikio makubwa Tanzania, inaingia katika msimu mpya wa michuano ya CAF ikiwa na matarajio ya kufanya vizuri na kuendelea kujiimarisha katika soka la Afrika.

Jumamosi Septemba 5, 2026, Yanga itakuwa ugenini nchini Botswana kukabiliana na Gaborone United, kisha kurudiana jijini Dar es Salaam Septemba 12, 2026 ikiwa ni hatua ya awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika.