Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Eto'o anusurika kifo ajalini

NKONGSAMBA, CAMEROON. STAA wa zamani wa Barcelona na Cameroon, Samuel Eto'o amelazwa hospitali baada ya kupata majeruhi kichwani kufutia ajali ya gari iliyotokea kwao Cameroon, imeripotiwa.
Jarida la France Football limeripoti kwamba mshambuliaji huyo aliyewahi kuzichezea pia Inter Milan, Chelsea na Everton alihitaji kufanyiwa vipimo zaidi baada ya gari yake kugongana na basi.
Ajali hiyo imetokea karibu na mji wa Nkongsamba huko Cameroon, wakati Eto'o alikuwa akiiendeesha akitokea harusini.
Mwandishi wa habari, Martin Camus alizungumza na Eto'o, ambaye alitaka kuwaondoa hofu watu kwa kuwahakikishia kwamba anaendelea vizuri. Picha zilionyesha jinsi gari la Eto'o lilivyoharibika kutokana na ajali hiyo.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, hakuna kifo chochote kilichoripotiwa kwenye ajali hiyo kwa mujibu wa BBC baada ya kuzungumza na moja ya ndugu wa mwanasoka huyo.
Eto'o alistaafu soka mwaka mmoja uliopita baada ya kupata mafanikio makubwa akipita kwenye timu kibao ikiwamo Real Madrid, Barcelona, Inter Milan na Chelsea kwa kuzitaja kwa uchache huku akibeba mataji mengi ikiwamo matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Alibeba pia medali ya Dhahabu ya Olimpiki na alishinda ubingwa wa Afcon akiwa na kikosi cha Camerroni mwaka 2000 na 2002. Eto'o amekifungia kikosi cha Indomitable Lions mabao 49 katika mechi 97.