Duchu arudishwa Simba
SIMBA ina mpango wa kumrudisha beki wake wa zamani David Kameta “Duchu” ambaye alikuwa akiichezea Mtibwa kwa Mkopo.
Duchu aliitumikia Simba na baadaye akapelekwa kwa mkopo Geita kabla ya kuhamia Mtibwa Sugar ambapo mkataba wake na Simba ulitarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Hivi karibuni inaelezwa kuwa Simba walizungumza na Duchu na kumpa mkataba wa miaka miwili na sasa amemaliza mkataba wake wa mkopo na Mtibwa Sugar na kurudishwa klabuni ambapo msimu ujao atawania namba na Shomary Kapombe.