Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Simba Day inavyoibua mastaa

MASTAA Pict

Muktasari:

  • Katika tamasha la mwaka jana, jina la Rushine de Reuck ndilo lililotikisa kutokana na kiwango bora alichoonyesha Simba ikicheza na Gor Mahia kwenye Uwanja Benjamin Mkapa.

KILA mwaka tangu 2009, katika mechi ya kirafiki kwenye Tamasha la Simba Day kumekuwa na mmoja wa wachezaji anayeibuka na kuwa gumzo.

Katika tamasha la mwaka jana, jina la Rushine de Reuck ndilo lililotikisa kutokana na kiwango bora alichoonyesha Simba ikicheza na Gor Mahia kwenye Uwanja Benjamin Mkapa.

Beki huyo raia wa Afrika Kusini alijiunga na Simba akitokea Mamelodi Sundowns na aliletwa na Kocha Fadlu Davids na hadi sasa anaendelea kukipiga akitarajiwa kuonyesha moto katika mechi ya leo dhidi ya Kenya Police ya Kenya.

Usajili wake unatajwa ni moja ya bora kufanywa na Simba na kama alivyoibeba msimu uliopita, anatarajiwa kufanya hivyo msimu unaotarajiwa kuanza Agosti 14.

Hapa tunakuletea nyota walioibika gumzo baada ya mechi ya Simba Day.

MASTA 01

MORICE ABRAHAM

Kiungo huyo kwanza alianza kumvutia Fadlu wakati alipoomba kufanya mazoezi na Simba kisha kocha huyo kufanya maamuzi ya kumsajili moja kwa moja.

Hata hivyo, alionyesha kiwango bora kwenye mechi ya kirafiki ya Simba Day kwa dakika 45 tu alizopewa.

Ni miongoni mwa vijana wachache waliofanikiwa kucheza  FK Spartak Subotica ya Serbia aliwahi kwenda kwa mkopo kwenye RFK Novi Sad akiwa bado kijana mdogo na kupata malezi ya soka la kulipwa.

Mchezaji huyo anacheza zaidi nafasi ya kiungo mshambuliaji, pia anaweza kutumika pembeni kama winga kutokana na uwezo wake wa kumiliki mpira na kutengeneza nafasi.

MASTA 02

DEBORA FERNANDEZ

Fernandez ni mmoja wa wachezaji wa kigeni waliowahi kutambulishwa Simba Day na kuonyesha kiwango bora siku hiyo kiasi cha mashabiki kuanza kuliimba jina lake.

Tangu hapo kocha huyo alikuwa akimpa nafasi ya kuanza mara ya kwanza kwenye mashindano ya ndani na yale ya kimataifa lakini baadae akashindwa kuhimili presha ya ushindani wa namba iliyokuwepo kikosini hapo.

MASTA 03

AUGUSTINE OKRAH

Ndiye aliyeibuka gumzo katika mechi ya Simba Day ilipocheza dhidi ya St George ya Ethiopia. Licha ya kutotupia, alionyesha kiwango bora na hivyo, Simba kuonyesha haikukosea kumsajili kutoka Bachem United, alikofunga mabao 14 na kutoa pasi mbili (asisti) katika michezo 32 ya Ligi Kuu Ghana na kuiwezesha timu hiyo kumaliza nafasi ya tatu nyuma ya Medeama na mabingwa, Asante Kotoko.

Hadi Okrah anaondoka Simba msimu wa 2023/24, hakupata nafasi ya kucheza mara kwa mara akifunga mabao manne ya Ligi Kuu Bara.

MASTA 04

BERNARD MORRISON

Morrison ambaye kwa sasa yuko nchini alitua kwa mara ya kwanza mwaka 2020 na kujiunga na wananchi Yanga akiwa mchezaji huru, usajili ambao ulikuwa na misukosuko ya mikataba baina yake na mabingwa hao watetezi.

Alikuwa tayari anajulikana baada ya kucheza Yanga lakini tamasha hilo lilimpa jukwaa kubwa zaidi kutokana na kile alichokifanya uwanjani na vituko vyake nje ya uwanja.

Licha ya kutua Simba ila nyota huyo alidumu kwa msimu mmoja na nusu na alirejea tena Yanga kwa mara ya pili na msimu 2023/24 kwenye Ligi Kuu Bara alifunga mabao matano.

MASTA 05

SHIZA KICHUYA

Kichuya alijizoelea umaarufu kwenye tamasha hilo kwa mara ya kwanza alipojiunga na Simba mwaka 2016 akitokea Mtibwa Sugar.

Winga huyo alifanya vizuri na alikaa Simba hadi mwaka 2019 akaanza kutolewa kwa mkopo kwenye Klabu za Pharco na Enppi SC za Misri na baada ya kurejea tu nchini mwaka 2020 alijiunga na Namungo, JKT Tanzania na sasa Coastal Union.

MASTA 06

MOSES PHIRI

Raia huyo wa Zambia alijiunga na Simba rasmi Juni 15, mwaka 2023 akitokea Zanaco FC, ya kwao na alimaliza nafasi ya pili kwa ufungaji na mabao 14 nyuma ya mfungaji bora Ricky Banda aliyemaliza na 16. Katika tamasha la mwaka 2023 Phiri pia alifanya vizuri na hadi kwenye Ligi Kuu Bara na msimu ulioisha alifunga mabao 10 nyuma ya, Saidi Ntibazonkiza ‘Saido’ na Fiston Mayele waliofunga 17.

MASTA 07

MEDDIE KAGERE

Mshambuliaji huyo mzaliwa wa Uganda mwenye uraia wa Rwanda, katika msimu wake wa kwanza wa 2018/2019, alikuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu Bara akifunga mabao 23 na kama haitoshi aliendelea kutawala tena kwani msimu wa 2019/2020 aliibuka kidedea baada ya kufunga mabao 22.

Baada ya kuitumikia Simba misimu minne rasmi nyota huyo mwaka jana aliagwa kwa heshima katika tamasha hilo na kutimkia Singida Fountain Gate na msimu uliopita alifunga mabao manane ya Ligi Kuu Bara.

MASTA 08

EMMANUEL OKWI

Mara ya kwanza kwa nyota huyo kutua nchini ilikuwa mwaka 2010 na alijiunga na Simba akitokea SC Villa ya Uganda.

Katika tamasha la pili la Simba Day mwaka 2010, aliibuka shujaa licha ya suluhu dhidi ya Express FC ya Uganda.

Umahiri wake kwenye kufunga msimu huo uliiwezesha Simba kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara kwa mara ya kwanza baada ya kutawaliwa na mahasimu wao Yanga waliotwaa mara tatu mfululizo kuanzia 2014/15, 2015/16 na 2016/17.