Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dube aendelea kutwaa mataji Hardrock FC

DUBE Pict

Muktasari:

  • Katika mchezo huo uliofanyika Novemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa Chahwanda uliopo mjini Kwekwe, Zimbabwe, Dube alifunga mabao dakika ya 47 na 62. Mengine ya Hardrock yalifungwa na Sizwe Khumalo dakika ya 39 na Nigel Matinha dakika ya 45.

ALIYEKUWA mshambuliaji wa Yanga, Prince Dube, ameendelea kung'ara akiwa na Hardrock FC ya kwao Zimbabwe baada ya kuifungia mabao mawili katika ushindi wa 4-0 dhidi ya Highlanders FC, uliowapa ubingwa wa Chibuku Super Cup.

Katika mchezo huo uliofanyika Novemba 28, 2026, kwenye Uwanja wa Chahwanda uliopo mjini Kwekwe, Zimbabwe, Dube alifunga mabao dakika ya 47 na 62. Mengine ya Hardrock yalifungwa na Sizwe Khumalo dakika ya 39 na Nigel Matinha dakika ya 45.

Hilo ni taji la pili kwa Dube tangu alipojiunga na Hardrock FC Julai 2, 2026, akitokea Yanga. Awali, aliiwezesha timu hiyo kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Zimbabwe msimu wa 2026.

DUB 01

Katika mchezo wa mwisho wa ligi hiyo dhidi ya FC Platinum, uliofanyika Novemba 21, 2026, Dube alifunga bao pekee dakika ya pili na kuihakikishia Hardrock ushindi wa 1-0 uliowapa ubingwa baada ya kufikisha pointi 73.

Hardrock FC, iliyopanda daraja msimu huu chini ya Kocha Mkuu, Kelvin Kaindu, ilijihakikishia ubingwa katika mchezo wake wa mwisho, ikimaliza kwa tofauti ya pointi mbili mbele ya mabingwa watetezi Scottland FC, iliyoshika nafasi ya pili kwa pointi 71.

Dube aliondoka Yanga baada ya kuitumikia na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu wa 2025-2026. Licha ya kuwa na ofa mbalimbali kutoka kwa klabu zilizohitaji huduma yake, aliamua kujiunga na Hardrock FC ya nyumbani Zimbabwe.

Nyota huyo alijiunga na Yanga Julai 6, 2024, akitokea Azam FC na kufanikiwa kutwaa mataji mbalimbali, yakiwamo ya Ligi Kuu Bara mara mbili mfululizo, akiwa mmoja wa washambuliaji tegemeo wa kikosi hicho.

Katika misimu yake miwili aliyoichezea Yanga, Dube alihusika katika mabao 37 ya Ligi Kuu Bara. Msimu wa 2024-2025 alifunga mabao 13 na kutoa asisti nane, huku msimu wa 2025-2026 akifunga 10 na kutoa asisti sita.

DUB 02

Msimu wake bora katika Ligi Kuu Bara ulikuwa 2020-2021, alipokuwa akiichezea Azam FC baada ya kujiunga nayo akitokea Highlanders ya Zimbabwe. Katika msimu huo, alionyesha kiwango bora na kumaliza nafasi ya tatu katika orodha ya wafungaji bora.

Dube aliifungia Azam FC mabao 14 ya ligi, akizidiwa na Chris Mugalu aliyefunga 15 na John Bocco aliyekuwa mfungaji bora kwa mabao 16, wote wakiitumikia Simba.