Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dodoma yaipania Yanga

KOCHA Mkuu wa Dodoma Jiji, Mbwana Makata amesema wana kila sababu ya kutoka na pointi tatu katika mchezo wao dhidi ya Yanga utakaochezwa kesho Jumamosi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, jijini hapa.

Akizungumza na Mwanaspoti baada ya kumalizika mazoezi leo Ijumaa mchana, Makata amesema amekiandaa kikosi chake vizuri kuhakikisha wanapata matokeo mazuri katika mchezo huo.

"Nimekiandaa vizuri kikosi changu katika mchezo huo na morali ya wachezaji ipo vizuri kuhakikisha tunapata matokeo ya pointi tatu," amesema Makata

Makata amesema anajua kwamba wapinzani wao wamekuwa bora msimu huu kutokana na kuongoza ligi mpaka sasa.

"Tunafahamu kwamba Yanga hawajapoteza mchezo wowote mpaka sasa, msimu huu wameimarika zaidi na kuwa katika timu bora, Yanga wana ubora mkubwa pamoja na mapungufu, tutatumia vyote hivyo kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,"

Naye nahodha wa timu hiyo, Mbwana Kibacha amesema mchezo huo ni muhimu ili kupata pointi tatu na kusogea nafasi za juu.

"Tunajua Yanga ni timu nzuri na kubwa, lakini tunahitaji pointi tatu kwa sababu hatujatofautiana sana pointi katika msimamo."

Kibacha aliongeza kwa kusema "Mechi hizi wachezaji binafsi huwa tunajiandaa vizuri zaidi, unajua mechi za Simba na Yanga ndio sehemu ya kuonekana,".