Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Dakika 28 za moto DJ Ally B akipagawisha Yanga Day

Muktasari:

  • Ally B aliingia kwenye shoo hiyo akiwa amevalia kipensi cheusi huku akiwa bila fulana akipiga nyimbo tofauti zenye mchenganyiko wa Bongo Fleva na Singeli.

DJ Ally B amefanya shoo kali kwenye kilele cha Yanga Day akifanya shoo kali ya kupiga muziki, kucheza na kuweka vichombezo.

Ally B aliingia kwenye shoo hiyo akiwa amevalia kipensi cheusi huku akiwa bila fulana akipiga nyimbo tofauti zenye mchenganyiko wa Bongo Fleva na Singeli.

Achana na kupiga muziki huo, Ally B ameonyesha umahiri mkubwa wa kucheza akiondoka kwenye steji na kuwafuata mashabiki pembeni ya majukwaa na kuimba nao.

Ally B ametumia dakika 28 kupiga shoo hiyo kali kwenye Uwanja wa Uhuru, akipiga jumla ya nyimbo 19 tofauti.

Wakati wote Ally B akiwa kwenye shoo hiyo, mashabiki wengi majukwaani wamekuwa wakipagawa kwa furaha wakicheza na kuimba kwa kufuatisha nyimbo hizo.

Yanga imekuwa ikimtumia DJ Ally B kwa mara ya tatu sasa mfululizo kwenye matamasha ya namna hii na hata baadhi ya mechi za kimataifa.

Mara baada ya Ally B kumaliza shoo hiyo, mashabiki walionekana kukaa chini kwenye viti wakipumzika baada ya dakika 28 za moto za kucheza kwa vaibu kubwa.