Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Deogratius Mafie anukia Pamba Jiji

Muktasari:

  • Akizungumza na Mwanaspoti, Mafie alisema mkataba wake na Kagera Sugar umeisha baada ya msimu wa 2025-2026 kumalizika na sasa anaangalia changamoto sehemu nyingine mpya, ambapo tayari mazungumzo rasmi na baadhi ya klabu nyingine yanaendelea.

KLABU ya Pamba Jiji iko katika hatua za mwisho za kufikia makubaliano ya kumsajili mshambuliaji, Deogratius Mafie baada ya nyota huyo kuamua kuachana na kikosi cha Kagera Sugar alichokiwezesha kupanda Ligi Kuu Bara kwa msimu wa 2025-2026.

Akizungumza na Mwanaspoti, Mafie alisema mkataba wake na Kagera Sugar umeisha baada ya msimu wa 2025-2026 kumalizika na sasa anaangalia changamoto sehemu nyingine mpya, ambapo tayari mazungumzo rasmi na baadhi ya klabu nyingine yanaendelea.

“Ni kweli nimefikia uamuzi wa kuondoka na nipo tayari kwa ajili ya kutafuta changamoto mpya, mazungumzo ya kuongeza tena mkataba mpya wa kuichezea Kagera Sugar yalikuwepo, ila nimeona ni muda mzuri wa kwenda sehemu nyingine,” alisema Mafie.

Licha ya kauli ya nyota huyo, ila Mwanaspoti linatambua, Mafie aliyechezea pia Biashara United, yupo katika hatua za mwisho za kujiunga na kikosi cha Pamba Jiji, baada ya pande zote mbili kufikia makubaliano mazuri.

Akizungumza na Mwanaspoti, Kaimu Mtendaji Mkuu wa Pamba, Ezekiel Ntibikeha alisema usajili wa timu hiyo kwa msimu ujao wa 2026-2027, umekamilika kwa kiasi kikubwa, japo jambo lililobakia kwa sasa ni kazi ya idara ya habari kuwatangaza tu.

Hata hivyo, licha ya kauli ya kiongozi huyo, Mwanaspoti linatambua Mafie anakaribia kujiunga na Pamba Jiji akitokea Kagera Sugar, akiungana na nyota wengine wapya, wakiwemo kipa, Steve Ochieng aliyetokea Shabana FC ya kwao Kenya.

Wengine ni Erick Johola kutoka Mashujaa FC, Nonyem Okorocha (Mlandege FC), Frank Ernest (KMC FC), Ally Saleh Machupa ‘Machupa JR’ (Namungo FC), Salehe Karabaka (Simba), Fadhili Baluba (Raskazone FC) na John Ochieng kutokea Zanaco FC.

Nyota wengine ni beki wa kulia, Abdallah Said Ali ‘Lanso’ na Mkongomani Malanga Horso Mwaku wote kutokea Singida Black Stars, ingawa kwa mshambuliaji huyo atajiunga na Pamba Jiji kwa mkopo wa msimu wa 2026-2027 na sio kuuzwa moja kwa moja.