Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Daraja la Kwanza Unguja yaanza kwa kishindo

UNGUJA Pict

Muktasari:

  • Kundemba ilipokea kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na Hassan Ali dakika ya pili ya mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Mao A, Mjini Unguja.

LIGI ya Daraja la Kwanza Kanda ya Unguja imeanza rasmi kwa mechi nne huku tatu zikianza na ushindi ikiwemo Ujamaa, Paje Star na Kitope.

Kundemba ilipokea kichapo cha bao 1-0 lililofungwa na Hassan Ali dakika ya pili ya mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa Mao A, Mjini Unguja.

Katika mechi nyingine kwenye Uwanja wa Matemwe, Mkoa wa Kusini Unguja, Ujamaa iliikaribisha Ranger Bulls kwenye ligi hiyo baada ya daraja kwa kuifunga mabao 2-1.

Katika mechi hiyo, Mohammed Rajabu aliitangulizia bao timu ya Ujamaa dakika ya 24 huku Filipo Mungala wa Ranger akiweka mzani sawa dakika ya 62 kabla Omary Mohammed hajaongeza bao la pili dakika ya 65.

Mechi nyingine, iliyochezwa uwanja wa Kitope, Kaskazini Unguja, Kitope iliibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Muungano Ranger na mabao yote yalifungwa na Hadhir Ahmada.

Katika hatua nyingine, New City na Sebleni United zilitoka sare ya bao 1-1 kwenye Uwanja wa Mao B, Unguja na Jairan Nguzo wa New City aliitanguliza kwa bao dakika ya 20, kabla ya Iddi Mgeni kusawazisha dakika ya 70.

Mzunguko huo uliendelea Septemba 22, na New King iliyoshuka daraja iliifunga Bridge bao 1-0 lililofungwa na Mundhir Khamis '44', huku Taifa Jang'ombe ikishinda 2-0 ya dhidi ya Kikungwi na mabao yote yalifungwa na Kassim Majid dakika '45+1' 86'.  Mundu na Villa zilitoa sare ya bao 1-1, huku Bweleo na Negro United zilimaliza dakika 90 bila kufungana (0-0).