Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Zanzibar kutangaza utamaduni kupitia AFCON

Muktasari:

  • Kauli ya waziri huyo imekuja wakati huu ambao umebaki takribani miezi sita kabla ya kufanyika kwa mashindano hayo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

WAZIRI wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Riziki Pembe Juma, amewasisitiza wananchi kisiwani hapa kutumia utamaduni wa Kizanzibari kuhakikisha wanautangaza kwenye mashindano ya Kombe la Mataifa Afrika (AFCON 2027).

Kauli ya waziri huyo imekuja wakati huu ambao umebaki takribani miezi sita kabla ya kufanyika kwa mashindano hayo katika nchi za Tanzania, Kenya na Uganda.

Waziri Pembe aliyasema hayo katika ufunguzi wa Tamasha la 31 la Utamaduni wa Zanzibar lililofanyika ukumbi wa Baraza la Wawakilishi, Wete, Pemba.

Alisema ni wajibu wa kila mmoja kuhakikisha mila, silka na utamaduni unalindwa, kuhifadhiwa na kuendelezwa kwa kuzingatia maadili ya Mzanzibari.

“Kaulimbiu yetu ni utamaduni wetu ni urithi wetu kwa vizazi vyetu, tumia fursa za utamaduni kwenye Afcon 2027, hivyo jamii inapaswa kuzitumia fursa mbalimbali za kiuchumi zitakazotokana na ujio wa mashindano ya AFCON 2027,” alisema.

 Naye Mkuu wa Wilaya ya Wete, Abdalla Rashid, alisema ujio wa mashindano ya AFCON 2027 ni fursa kwa Zanzibar kuutangaza utamaduni wake kwa wageni watakaofika nchini hapa. Alisema, ni muhimu kutumia fursa hiyo kuutangaza utamaduni huo ili hata baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, utamaduni wa Zanzibar uwe umetangazwa duniani kote.

AFCON 2027 itakayoanza Juni 19, 2027 hadi Julai 17, 2027 kwa Tanzania imepangwa kuchezwa kwenye viwanja vya Benjamin Mkapa (Dar es Salaam), Uwanja wa Samia Suluhu Hassan (Arusha) na Fumba (Unguja).