Dar City yatetea ubingwa wa BDL
Muktasari:
- Viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Maji, Juma Aweso, Waziri wa Kilimo, Daniel Godfrey Chongolo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mohamed Mwinjuma 'Mwana FA' na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabeet.
TIMU ya Dar City imetetea ubingwa wake wa Ligi ya Kikapu ya Dar es Salaam (BDL), baada ya kushinda michezo mitatu mfululizo kati ya mitano dhidi ya Stein Warriors.
Katika fainali hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa International School Of Tanganyika (IST), Masaki, jijini, Dar es Salaam, Dar City imeshinda michezo mitatu mfululizo iliyowafanya kutetea taji hilo ililolichukua mwaka jana 2025.
Dar City imeibuka mabingwa wa fainali hiyo iliyochezwa michezo mitatu kati ya mitano iliyopangwa kuchezwa, ambapo kwa sheria za Mpira wa Kikapu, michezo miwili iliyobakia haiwezi kuipa ushindi timu ya Stein Warriors.
Dar City iliingia fainali ikiwa na rekodi ya kushinda michezo yote 15 ya hatua ya ligi ya kawaida, kwani iliifunga JKT katika robo fainali na kuiondoa Vijana City Bulls katika nusu fainali, hivyo kufuzu kucheza mechi za kuwania taji.
Katika fainali ya leo mgeni rasmi ni Makamu wa Rais, Deogratius John Ndejembi, aliyeambatana na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda.
Viongozi wengine waliohudhuria ni Waziri wa Maji, Juma Aweso, Waziri wa Kilimo, Daniel Godfrey Chongolo, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Hamis Mohamed Mwinjuma 'Mwana FA' na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Hasheem Thabeet.