Hello

Your subscription is almost coming to an end. Don’t miss out on the great content on Nation.Africa

Ready to continue your informative journey with us?

Hello

Your premium access has ended, but the best of Nation.Africa is still within reach. Renew now to unlock exclusive stories and in-depth features.

Reclaim your full access. Click below to renew.

Coast vs Congo Kesho Uwanjani

Kipa wa zamani wa Harambee Stars na AFC Leopards, Mahmoud Abbas `Kenya One'(kushoto) akiwapa mawaidha wachezaji jinsi ya kucheza soka litakalowaburudisha watazamaji wakati wa mechi iliyochezwa Uwanja wa Khadija mjini Mombasa. Abbas alikuwa kwenye kampeni ya kumpigia debe mgombea uenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (KFF), Twaha Mbarak. PICHA NA ABDULRAHMAN SHERIFF

MWANDISHI WETU TIMU ya Coastal Union kutoka Tanga itapambana na Congo United kwenye mchezo wa kirafiki wa kujipima nguvu utakaofanyika kwenye uwanja wa Mbaraki Sports Club mjini Mombasa kesho Jumatano. Timu hizo mbili zinatarajia kuwapa burudani mashabiki wa soka wa Pwani kwani Congo na Coastal ya Tanzania zinacheza soka karibu inayofanana ya kutandaza boli chini na pasi fupi fupi. Timu ya Coastal Union imepiga kambi mjini Mombasa kujiandaa kwa msimu mpya wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara hali Congo United inaendelea kushiriki Ligi Kuu ya Kenya (KPL) ambapo mpaka sasa bado haijaimarika. Naibu mkufunzi wa Coastal Union, Shamsuddin Hussein amesema kwamba watachezesha kikosi imara kwenye mechi hiyo ambayo huenda ikawa ya mwisho katika maandalizi ya kambi yao hiyo. Katika mchezo wao wa kwanza w2a kirafiki mjini Mombasa, Coastal Union ilitoka sare ya kufungana bao 1-1 na wawakilishi wengine wa Pwani katika KPL, Bandari FC. ìTunaridhishwa na jinsi wachezaji wetu walivyojitayarisha kwenye mazoezi ya hapa Mombasa na kuwa katika hali nzuri,î akasema Hussein ambaye zamani alikuwa mshambuliaji mahiri wa klabu iliyokuwa maarufu mkoani Pwani ya Liverpool FC.